Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Atatufanya tumweke kwa ignore list ashindwe kuonekana....
Tuseme ule ukweli ambao mleta mada hajauongelea. Kuna hii tabia ambayo bibie mmoja alimkosoa sijui baada ya hapo kama urafiki uliendelea. Ana tabia ukianzisha uzi either atakuja kujibu kwa kuweka link ya uzi wake ambayo haufanani sana na wa mleta mada(hapa anakosea maana badala ya wachangiaji kuchangia uzi husika wanahamia kwenye link ya uzi wake)
Tabia ya pili,ukianzisha uzi ukanoga akaja changia kidogo tu atasema ataeleza kwa upana kwenye uzi wake atakaouanzisha badala ya huo(hio inaua uzi husika wadau wanabaki kusubiria uzi wake)

Huyo bibie alianzisha uzi,jamaa akaleta link yake hapo,sasa mwenye uzi alikua anahitaji mawazo mbali mbali akaomba link hio ifutwe itahamisha mjadala
 
Hapo mwanzo mi binafsi nilidhani tatizo lake ni makala zake tu ambazo mtu unaweza kuzipitia mbali.
Lakini kwa maelezo ya Numbisa kumbe jamaa pia ana tabia ya kuvamia thread za watu na kuhamisha wachangiaji kwa lengo la kujiona kuwa yeye ni "Kilongola" wa kujenga hoja, hivyo ndiye pekee anastaili kusikilizwa hapa Jf.
Kwa tabia hiyo nadhani waliofanyiwa hivyo yafaa wamkanye ikibidi kumzodoa ili akome mienendo yake isiyofaa.
Ni ushauri tu
Japo ni hivyo lakini pia kuna social intelligence - kujua useme nini na wakati gani ili uendane na watu waliokuzunguka. Mf. Darasani na hata mkutanoni. Ni haki ya kila mtu kusema lolote na cho chote lakini kama mtu yule yule ndiyo anaongea tu muda wote na kujifanya anajua kila kitu, hakanyiki wala kusikiliza hoja za wengine hata ziwe nzuri namna gani kunakuwa na mushkeli mahali. Kuwakwaza watu siyo lazima uvunje sheria kwa sababu maingiliano na watu katika nyanja zote hayajatungiwa sheria za vitabuni.

Hivyo kuwa na uhuru wa kuandika na kusema cho chote haina maana kweli ndiyo useme na kuandika cho chote hata katika masuala usiyoyajua sawa sawa huku ukipuuzia maoni ya wengine (pengine wenye ujuzi zaidi kuhusu mada husika). Hayo ni matumizi mabaya ya uhuru [emoji2221][emoji2221][emoji2221]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo yote utayapata ofisini kwetu.
Karibu mtaa wa Mkwepu Dsm, utaelezwa utaratibu mzima wa kufika kilele cha Kibo au Mawenzi[emoji23][emoji23]
Tunakuahidi kukufikisha vilele hivyo kwa amani huku ukifurahia hali ya hewa ya Kilimanjaro.
Karibu
Enhe hebu elezea utatufikishaje juu kote huko? Anza safari inapoanzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom