Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hivi karibuni pamekuwa na mvua,baadhi yetu watanzania tumejenga kwenye maeneo yenye mikondo ya maji ,mikondo ya maji haizibwi, inapokuja kuwachukua inabaki kupiga kelele ni mafuriko, mafuriko mnajifurika wenyewe, hutaki kujenga kwenye mlima unakwenda kujenda kwenye bonde”.JPM
 
Juzi nilikuwa namskia Mh Jafo, mtu mmoja kule Kilosa nafikiri alichana kitabu kitakatifu, nakushukuru umechukua hatua ya kumsimamisha kazi, lakini mimi namfukuza moja kwa moja muandikie barua ya kuondoka, ashinde kesi asishinde huyo si mfanyakazi wa serikali" - Rais
@MagufuliJP
 
Tuzitumie hizi mvua kama fursa, badala ya kulalamika, tuyatumie maji yaliyoletwa na Mungu kulima, tumekalia kulalamika mafuriko mafuriko na hatulimi, maji yakipotea tuanze kulalamika njaa, Mungu atashangaa alituletea maji hatukuyatumia, kila Mtanzania pale alipo afanye kazi”-JPM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…