Solskjaer, ambaye usiku wa kuamkia leo Ijumaa aliiongoza timu yake kwenye pambano la Europa League dhidi ya Club Brugge, alisema: “Marcus (Rashfor) atakuwa nje kwa miezi kadhaa.
Amefanyiwa vipimo na jeraha ni kubwa kuliko tulivyodhani awali. Natumaini atacheza msimu huu kabla haujaisha na kama hilo likitokea itakuwa katika mechi za mwisho kabisa za msimu.
Rashford, 22, ambaye amekuwa akivaa kifaa maalumu mgongoni kumsaidia kuweza kutembea. Aliumia kwenye mchezo dhidi ya Norwich, Januari 11, kisha akajitonesha siku nne baadaye baada ya kuingia uwanjani kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya Wolves.
Solskjaer amekiri alikosea kumuingiza kwenye pambano dhidi ya Wolves, lakini anadai Rashford mwenyewe alikomaa kutaka kucheza mechi hiyo akidai alikuwa fiti.
Solskjaer alisema: “Alikuwa fiti kabisa siku chake kabla ya tukio la kuumia na mimi si daktari wa kujua kama hakuwa vizuri, hivyo sikujua kama alihitaji muda zaidi kupona kabisa.”
In 2015, a guide dog named Figo was given the ASPCA's "Dog of the Year" award for throwing himself in front of an oncoming bus to protect his blind owner in New York. He didn't leave her side until she received medical attention, even though his leg was broken.