Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwingine anaweza asitake kufikiria au hata akawa anaogopa kuwaza vitu ambavyo pengine vyaweza kumuumiza au kumgharimu zaidi kwa sasa. Yaani kwa ufupi haoni umuhimu wa kuwa na mpango mbadala kwa kuwa sasa mpango huu unafanya kazi sawasawa.
 
Ndugu yangu hebu fikiria hata pale inatokea mtu ameondokewa na mtu aliyempenda au niseme aliyekuwa anamtegemea sana wengi hulia au kuumia na kukata tamaa. Ukifuatilia wengi hawalii kwa kuwa wanaumizwa sana na kifo cha mpendwa wao, wengi hulia kwa kuwa sasa wanawaza itakuwaje? Maisha yataendaje bila yule mtu?
 
Maana walimtegemea yule kwa asilimia zote mia moja, hawakuwahi fikiri kinyume na kujipanga endapo itatokea hivyo. Ukiangalia mtu anapofariki wengi hulia sana na kuumia sana kwa kuwa wanaona ndoto zao zimekomea pale, maana waliweka matumaini kwa mtu yule, au mwingine ni biashara imeungua moto au ameibiwa , kila kitu huishia hapo maana hakuwahi kuwa na mipango endelevu ikiwa hali kama hiyo itatokea.
 
Hakuwahi kuwaza hayo au pengine hakuwahi kukutana na mtu wa kumpa changamoto kama hizo, hakuwahi kuwa katika mazingira ya kumfanya awaze hivyo. Maana kuna watu wengine ukimwambia kuhusu haya mambo atakuambia kwa nini unawaza mabaya, ni kweli inaweza isikifurahishe kuwaza hivyo lakini kuogopa kwako kuwaza hivi haizuii hayo mambo kutokea, hivyo ni lazima uweke hofu pembeni na kufikiria nini kifanyike endapo yatakukuta hayo.
 
Hebu jiulize hiyo biashara yako au ni hiyo nyumba je, umeikatia bima? Ndugu yangu unaweza ukaamua kukata bima kwa ajili ya hiyo biashara yako ili hata ilikotokea lolote basi usichanganyikiwe, usiwe mtu ambaye hujui uanzeje, usikimbilie kuangalia gharama ya hiyo bima au kusikiliza wanaokuambia kuwa unaweza kulipia na usikutwe na hayo matatizo na ukawa umepoteza pesa yako lakini ukikutwa je itakuwaje? Chukua hatua leo.
 
Ni ofisini kwako unatumia mifumo ya kompyuta kutunza taarifa nyingi kwa ajili ya shughuli zako za kila siku, hakikisha unatunza taarifa zako nje ya hapo ofisini kama mbadala ikitokea umevamiwa au jengo limeungua moto. Kama ni ofisi kubwa inabidi uwe hata na ofisi nyingine mahali pengine yenye kila kitengo maalumu ili shughuli nyingine ziendelee kama kawaida hata kama utapatwa na maafa makubwa.
 
Hakikisha unakuwa na utamaduni wa kutunza taarifa zako sehemu nyingine ambapo utaweza kuzipata kama hizi unazotumia sasa zitapotea au kuharibika.
Usiishi kwa kuweka matumaini kwa mtu mmoja tu, hata kama ni mtu unayeona ana uelewa mkubwa sana , hakikisha kama unaona ana uelewa wa vitu vingi basi hakikisha unahamisha uelewa alio nao kwa watu wengine pia ili hata asipokuwepo basi usiathirike na kutokuwepo kwake, ndio unamuamini sana lakini tambua huyo ni binadamu tu anaweza kuanguka tu na asiamke tena, utafanyaje?
 
Chukua hatua sahihi. Wengine wameweka matumaini yao yote kwa wazazi au ndugu fulani wanaoona wana uwezo wa kuwasaidia katika maeneo fulani, ndugu yangu, imewafanya hata kubweteka kwenye shughuli zao kwa kuwa wanaamini wapo watu wa kuwatimizia mahitaji yao, ni wanadamu tu hao kesho anaweza asiwepo utaishije? Amka, jifunze kusimama na kufanya mambo yako mwenyewe leo ili hata siku hawapo usiyumbe uweze kuendelea, maana tambua kuwa haijalishi utakutana na nini maisha huwa ni lazima yaendelee, yataendeleaje kama haujajipanga sawasawa?
 
Unao uwezo wa kusimama mwenyewe , unao uwezo wa kufanya hiyo shughuli, komaa acha kujishusha na kusubiri wengine wakufanyie. Kama unadhani ni lazima umtegee mtu basi ni vyema kama utaweka tumaini lako kwa Muumba wako maana yeye hafi, yupo milele huyo hatakuangusha kamwe.
 
Hapa magubike na maguha sijui Pana gundu gani aisee[emoji26]
Itabidi unifwate tu hukuhuku..ukifika hapa unaogelea kuja ng'ambo hii,nakuamini Wewe mwanaume wa shoka..umeongelea Hindi sembuse hapa kilosa[emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SHIMBA YA BUYENZE kaniletea kabati ya baridi....maana sasa hivi nakula barafu tu ndio napoza mwili.
Ushemeji ni kusaidiana shemeji langu la nguvu. Donti wori ezi longi ezi ai emu alaivu hutapata shida kamwe hata Mfilisti akisepa mazima. Everesingi wili bi OKE shemeji [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…