Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna kipindi walisema eti wanasayansi wanafanya kulisukumia liangukie Africa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sasa sijui kweli
Kulisukumia liangukie Afrika haitasaidia Moana. Kila kitu chenye uhai kitakufa tu labda viumbe wanaokaa vilindini na chini ya ardhi; na ambao hawategemei nishati ya jua kuendesha maisha yao.

Jiwe hili kubwa likigongana na dunia litakuwa na spidi kali na mgongano huu unaweza kuitetemesha dunia mpaka iyumbe yumbe kwenye mhimili wake. Hili pekee linaweza kuathiri mfumo wa majira na kuharibu hali ya hewa.

Mbali na mioto itakayowaka kwa muda mrefu, athari kubwa hata hivyo inatokana na vumbi litakalotimkia angani baada ya mgongano huu. Wanasema tani trillioni kadhaa za vumbi zitarushwa kwenye anga yetu na kubakia huko kwa miongo kama siyo karne kadhaa. Hii ina maana kwamba dunia haitapata mwanga wa jua na katika muda wote huo kutakuwa na giza totoro. Hii ina maana hakuna photosynthesis wala michakato mingine yote inayohitaji nishati ya jua. Na bila jua dunia yote itarudi kwenye ice age. Wanasema pengine itachukua miaka mitatu tu bila jua kwa viumbe wote kuteketea.

Kama hiyo haitoshi, vumbi hili litakuwa na charged particles na hii itasababisha radi kali na mvua za miaka na miaka. Kutakuwa na dhoruba kila kona. Isitoshe, charged particles hizi zitaingiliana na hata kuathiri magnetic field yetu ambayo kimsingi ndiyo hutulinda na nguvu za mnunurisho kutoka kwenye jua hasa wakati jua linaporipuka. Bila nguvu hizi kutakuwa na radiation surges ambazo zitakaanga kabisa mifumo yetu yote ya kielektroniki ikiwemo njia zote za kusafirisha na kutunza umeme.

Kwa ujumla dunia itageuka na kuwa hatarishi kwa uhai wetu na itachukua mamia ya miaka ili kurudia tena hali ya kawaida.

Jiwe lililowaua akina Dinosaur kule Yucatan Peninsula lilikuwa ni dogo tu likilinganishwa na huyu mnyama Apophis lakini wanasayansi wanaamini kuwa liliweza kuua zaidi ya asilimia 98% ya viumbe vyote vilivyo hai na dunia ilichukua zaidi ya miaka 300 kuweza kuanza kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida.

Haya ni mambo ya kutisha ambayo hayaelezeki japo wanazuoni wa mambo ya unabii wanaamini kuwa kila kitu kimeelezwa katika kitabu cha Ufunuo.
 
Aseeee
 
Ndiyo shida ya majanga bro, yanaleta taharuki sana pole pia kwa hilo, nimefurahi fahamu binti ni mpenda science [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545] bora uzima mashindano yatasubiri
Wenzetu hawa wanaona mbali sana bro. Wameshatabiri kuwa watakumbwa na upungufu mkubwa wa madaktari, wahandisi na wataalamu wa kompyuta huko mbele ya safari. Wameanzisha programu za kuwavutia watoto tangu wakiwa wadogo ili wapende mambo ya sayansi. Kamalaika kako haka kana ndoto ya kuwa pediatric neurosurgeon siku moja na kamo kwenye mchepuo huo. Tuendelee kukaombea bro [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…