Kulisukumia liangukie Afrika haitasaidia
Moana. Kila kitu chenye uhai kitakufa tu labda viumbe wanaokaa vilindini na chini ya ardhi; na ambao hawategemei nishati ya jua kuendesha maisha yao.
Jiwe hili kubwa likigongana na dunia litakuwa na spidi kali na mgongano huu unaweza kuitetemesha dunia mpaka iyumbe yumbe kwenye mhimili wake. Hili pekee linaweza kuathiri mfumo wa majira na kuharibu hali ya hewa.
Mbali na mioto itakayowaka kwa muda mrefu, athari kubwa hata hivyo inatokana na vumbi litakalotimkia angani baada ya mgongano huu. Wanasema tani trillioni kadhaa za vumbi zitarushwa kwenye anga yetu na kubakia huko kwa miongo kama siyo karne kadhaa. Hii ina maana kwamba dunia haitapata mwanga wa jua na katika muda wote huo kutakuwa na giza totoro. Hii ina maana hakuna photosynthesis wala michakato mingine yote inayohitaji nishati ya jua. Wanasema pengine itachukua miaka mitatu tu bila jua kwa viumbe wote kuteketea.
Kama hiyo haitoshi, vumbi hili litakuwa na charged particles na hii itasababisha radi kali na mvua za miaka na miaka. Kutakuwa na dhoruba kila kona. Isitoshe, charged particles hizi zitaingiliana na hata kuathiri magnetic field yetu ambayo kimsingi ndiyo hutulinda na nguvu za mnunurisho kutoka kwenye jua hasa wakati jua linaporipuka. Bila nguvu hizi kutakuwa na radiation surges ambazo zitakaanga kabisa mifumo yetu yote ya kielektroniki ikiwemo njia zote za kusafirisha na kutunza umeme.
Kwa ujumla dunia itageuka na kuwa hatarishi kwa uhai wetu na itachukua mamia ya miaka ili kurudia tena hali ya kawaida.
Jiwe lililowaua akina Dinosaur kule Yucatan Peninsula lilikuwa ni dogo tu likilinganishwa na huyu mnyama Apophis lakini wanasayansi wanaamini kuwa liliweza kuua zaidi ya asilimia 98% ya viumbe vyote vilivyo hai na dunia ilichukua zaidi ya miaka 300 kuweza kuanza kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Haya ni mambo ya kutisha ambayo hayaelezeki japo wanazuoni wa mambo ya unabii wanaamini kuwa kila kitu kimeelezwa katika kitabu cha Ufunuo.