Lakini, ili hili litokee lazima michuano ya Euro 2020 isifanyike ili kutoa nafasi kwa klabu kucheza mechi za ligi wakati wa kiangazi, maana kama michuano hiyo ikiwapo wachezaji watajiunga na timu zao za taifa na hawatapata nafasi ya kucheza soka katika ngazi ya klabu.
UAMUZI WA TATU:
Ligi kuisha hapa
Kama tatizo la Corona lisipomalizwa mapema basi mashabiki wengi wa Liverpool wanataka uamuzi huu ambao ni kumaliza ligi katika hatua hii na kuwapa ubingwa huku. Norwich City, Aston Villa and Bournemouth zikishushwa daraja.
Uamuzi huu unainufaisha zaidi Liverpool ambayo itapata ubingwa ambao inastahili, lakini unaziumiza timu nyingi, kuanzia zile zitakazoshushwa daraja wakati zikiwa na nafasi bado ya kupamba na kubaki Ligi Kuu hasa kutoka na ukweli kuwa tofauti kati ya timu ya 18 na ya 17 na 16 ni mabao tu.
Lakini pia timu ambazo zinapambana kutafuta nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, Manchester United, Wolves na Sheffield United zitaathiriwa na uamuzi huu kwa sababu bado zina nafasi ya kuingia nne bora kama ligi ikiendelea, lakini ikimalizwa hapa basi hawatashiriki michuano hiyo mwakani.
UAMUZI WA NNE: Kuongeza idadi ya timu
Ili kuepusha kelele ya timu zitakazoshuka daraja na pia kuiwezesha Liverpool kutwaa ubingwa ambao imeupigania sana msimu huu, basi Bodi ya Ligi inaweza kuamua hakuna kushusha timu daraja na kuipa ubingwa Liverpool.
Na ili kuzipa haki zile timu ambazo zimekuwa na msimu bora Ligi Daraja la Kwanza, timu za Leeds na West Brom zipewe nafasi ya kupanda daraja, hii itamaanisha kuwa msimu ujao utakuwa na timu 22 badala ya 20, huku kila timu ikifurahi, japokuwa zile za timu zinazowania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa zitalia lia tu.
Harry Kane, Gabriel Jesus, Mauro Icardi na Timo Werner wako katika mawindo ya Juventus. Ronaldo ametimkia nyumbani kwao Madeira muda mfupi baada ya Italia kukumbwa na maambukizi ya virusi vya corona.