Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lina Medina' kutoka nchini Peru' anatajwa kuwa mwanamke ambae alijifungua akiwa na umri mdogo zaidi. Alijifungua akiwa na miaka 5 miezi 7 na siku 21 tu. Inasemekana alibakwa lakini haijawahi kuthibitishwa au kufahamika zaidi sababu familia yake na yeye mwenyewe walikataa kuongea na vyombo vya habari. Bado yupo hai kwa sasa ana miaka 85.
Chanzo: The Sun
 
Charles Darwin' alimuoa binamu yake na kufanikiwa kupata watoto 10 ambapo 7 ndiyo waliweza kufikia mpaka utu uzima 3 walifariki. Charles aliona huenda kuna tatizo katika uzao wake akihusisha na undugu alionao na mke wake, alianza kufanya utafiti katika mimea. Alichogundua ili kupata uzao imara ni bora uchanganye mbegu tofauti kuliko ndugu wa uzao mmoja.
 
Tafiti: Wanaume ndiyo wanao ongoza kwa kusema " Nakupenda" kwa mara ya kwanza kuliko wanawake. Sababu zinatajwa nyingi lakini mojawapo wanaume husema hivyo ili kuaminiwa na mwenza wake haraka ili wafanye mapenzi mara ya kwanza haraka zaidi.
Chanzo: Psychology Today, Bustle...
 
Mwanaume kunyonya matiti ya mke/mpenzi hakufanyi kuepuka na saratani ya matiti kwa mwanamke bali Mama kumnyonyesha walau kwa mwaka mmoja mtoto husaidia kujiepusha na saratani hiyo.
Chanzo: Mwananchi
 
Rungrado May Day Stadium' kutoka Korea Ya Kaskazini ndiyo uwanja wa michezo ambao unaingiza mashabiki wengi zaidi kuliko viwanja vingine duniani. Unaweza kuingiza mashabiki mpaka 150,000, lakini wastani watu 114,000 ndiyo watakaa kwenye viti. Uwanja huo ulikamilika kujengwa mwaka 1989.
Chanzo: World Atlas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…