Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kabla hujatapika mwili huzalisha kwanza kiasi kikubwa cha mate kwaajili ya kulinda meno yasiyeyuke. Kuna asidi ambayo huzalishwa wakati unatapika bila mate meno yote yangeyeyuka.
 
Unaweza kwenda mbele ya muda na kurudi nyuma pia (Time Travelling), kwa nadharia za kisayansi inawezekana lakini haijawahi kufanyiwa majaribio sababu haiwezekani kutoka na ufinyu wa teknolojia. Mojawapo ya kigezo ni kuwa na chombo kitakachoweza kwenda na kufikia spidi ya mwanga (Light) ambayo ni 3000,000,000 m/s.Vyanzo: Medium, BBC, Express...
 
Tafiti: Watoto wanaozaliwa kutoka kwa wazazi ambao umri wao umeenda sana wana uwezekano mkubwa wa kuwa na nidhamu katika maisha yao tofauti wanaozaliwa na wazazi vijana. Sababu zinazotajwa wazazi ambao umri umeenda huwa ni wavumilivu, wanajiamini, uwepo wa mali (Pesa..) ambavyo ni muhimu kwa makuzi ya mtoto katika hali chanya zaidi.Chanzo: Heathline
 
Usipende kukaa muda mrefu chooni sababu ni hatari ya afya yako. Inashauriwa usizidishe zaidi ya dakika 5, sababu unaweza kupatwa na tatizo ambalo moja ya dalili zake ni kuvuja kwa kinyesi kitaalamu ugonjwa huo unaitwa Hemorhoids'

Chanzo: Mental Floss
 
Mkojo wa binadamu unatajwa kama ni mojawapo kinga na tiba ya magonjwa mbalimbali kama kuiweka ngozi yako kuwa na afya nzuri, kupunguza uzito, tiba ya haraka kwenye kidonda, tiba ya jino n.k. Lakini kisayansi hakuna uthibitisho wowote kuwa mkojo wa binadamu ni tiba.Chanzo: BBC
 
Wataalamu wa mazingira wamedai kupunguza ulaji wa nyama, na kula zaidi vyakula vitokanavyo na mimea kutasaidia kukubaliana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Hii ni kutokana na baadhi ya vyakula kuhitaji eneo kubwa, maji mengi, na hutoa gesi chafu wakati wa kuvizalisha na kuviandaa.
 
Back
Top Bottom