Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkurugenzi wa Ufundi wa PSG, Leonardo Araujo, alikaririwa akisema kuwa katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi Neymar atakuwa sokoni, huku kiwango cha ada ya kumnyakua kikiwa hakijawekwa bayana, lakini kinakadiriwa kuwa nusu ya ile Euro 222 milioni. iliyolipwa na PSG wakati wanamsajii kutoka Barcelona. Usajili huu unategemewa kusumbua kwani timu zinazomtaka zinatazamiwa kuongezeka na kuungana na Barcelona kwenye mbio hizo, kutokana na kauli ya Leonardo.
 
4. Paul PogbaKlabu zinazomtaka: Juventus, Real MadridKlabu aliyopo:Manchester UTDThamani yake: Euro 100 milioniHakuna ubishi kuhusu kiwango cha Mfaransa huyu. Amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia 2018 na hata kwenye klabu yake ya Manchester United. Amezivutia klabu kubwa nyingi ikiwa ni pamoja na Real Madrid, Juventus. Klabu hizi mbili zinaonekana kuwania saini ya kiungo huyu kwa udi na uvumba. Hali hii imesababisha Pogba kuwa kwenye orodha ya wachezaji watakaosumbua sana katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kulingana na timu zinazomuhitaji. Thamani yake kwenye soko la usajili kwa sasa ni Euro 100 milioni.
 
3. Lautaro Martinez

Klabu inayomtaka:FC BarcelonaKlabu aliyopo: Inter MilanThamani yake: Euro 80 milioniStraika huyu kwa sasa ana umri wa miaka 22 tu, tayari ameonyesha kiwango bora akiwa na timu ya Inter Milan, umri wake na kiwango chake vimesababisha kuivuta miamba mbali mbali barani Ulaya kuwania saini yake.
 
2. Jadon Sancho

Timu zinazomtaka: Man United, Chelsea, Liverpool, ReaL MadridTimu aliyopo: BorussiaDortmundThamani yake: Euro 133 milioniNi moja ya vijana wa miaka ya 2000 ambaye amekuwa na kiwango bora sana akiwa anakipiga na miamba ya soka ya Borussia Dortmund kule nchini Ujerumani. Ameonyesha kiwango cha hali ya juu sana kulinganisha na umri wake ambao ni miaka 19 tu, hivyo klabu nyingi zinapigana vikumbo kuwania saini yake kwani zinaamini watakuwa na uwezo wa kumtumia kwa muda mrefu. Klabu za Manchester United, Liverpool, Chelsea na Real Madrid zinatajwa kupigana vikumbo kuwania saini yake. Thamani yake sokoni kwa sasa ni Euro 133 milioni.
 
FB_IMG_1584610471784.jpeg
 
1. Timo WernerTimu zinazomtaka:Liverpool, BarcelonaTimu aliyopo: RB LeipzigThamani yake: Euro 80 milioniTimo ambaye ana miaka 24, anawindwa ile mbaya na klabu kubwa za Ulaya, baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu sana akiwa na RB Leipzig ya Ujerumani.
 
Back
Top Bottom