2. Jadon Sancho
Timu zinazomtaka: Man United, Chelsea, Liverpool, ReaL MadridTimu aliyopo: BorussiaDortmundThamani yake: Euro 133 milioniNi moja ya vijana wa miaka ya 2000 ambaye amekuwa na kiwango bora sana akiwa anakipiga na miamba ya soka ya Borussia Dortmund kule nchini Ujerumani. Ameonyesha kiwango cha hali ya juu sana kulinganisha na umri wake ambao ni miaka 19 tu, hivyo klabu nyingi zinapigana vikumbo kuwania saini yake kwani zinaamini watakuwa na uwezo wa kumtumia kwa muda mrefu. Klabu za Manchester United, Liverpool, Chelsea na Real Madrid zinatajwa kupigana vikumbo kuwania saini yake. Thamani yake sokoni kwa sasa ni Euro 133 milioni.