Wasp injector knife" kinatajwa kama mojawapo ya kisu hatari, ukichomwa na kuminya kitufe kilichopo juu ya kisu hicho hutoa gesi ya Co2 (hii huwekwa katika mshikio wake) na kutengeneza tufe mfano wa mpira wa Basketball' kisha hulipuka mfano kama bomu.
Namna unavyopenda kula kwa haraka zaidi, uwezekano wa kuongezeka uzito huwa mkubwa pia sababu kula haraka husababisha kula chakula kingi kuliko uhitaji wa mwili wako ubongo unashindwa kutambua kwa haraka kiasi cha chakula ulichokula (Unauchanganya ubongo)
Mwanaume huchukua muda mrefu zaidi kurudia kufanya mapenzi na mwanamke mmoja tu (aliyetoka kufanya nae mapenzi) lakini ana uwezo wa kuhamia kwa haraka kwa mwanamke mwingine mpya ndani ya muda mfupi kitaalamu inaitwa refractory period'
Unywaji wa soda yenye kiasi cha 600 ml kila siku inazeesha uwezo wa seli za damu kwa kiwango sawa na mvutaji wa sigara wa miaka 4 mpaka 6. Kama ni mtumiaji mkubwa wa soda hakikisha unapenda kunywa maji mengi pamoja na mazoezi.
Apple inasemekana wana kitengo cha siri cha usalama kwaajili ya kuwachunguza wafanyakazi kuhakikisha hakuna anaevujisha siri ya kampuni. Na hiyo ni mojawapo ya sababu ya kuwa na nafasi kubwa kuchaguliwa Chuo Kikuu Cha Havard' kuliko kuajiriwa na Apple'
Apple' wana sehemu maalum kwaajili ya kufanyia majaribio ya vifaa vyake (Prosesa, Chips n.k) kwa kuviweka katika hali ngumu mfano huviweka katika mazingira tofauti ya joto kuanzia -40° mpaka 110 ° sentigredi. Lengo kuangalia uimara, kama vikishindwa kuhimili katika sehemu hiyo maalum ya majaribio hawavitumii katika vifaa vyao kama simu, kompyuta n.k
Saikolojia: Unaweza kumtambua mtu anaekupenda kwa namna anavyozungumza na wewe. Kwa mwanaume hupenda kuongea kwa sauti ya chini na taratibu, wanawake huipamba sauti kuwa nyororo zaidi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.