Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anga la sayari ya Mars' ni nyembamba sana kiasi kwamba kama utahitaji kushusha chombo kikubwa kwa usalama mfano kama Gari la kawaida utahitaji ukubwa wa Parachuti yenye ukubwa sawa na Magari makubwa si chini ya 9. Na hiyo ndiyo sababu mpaka sasa ni kazi kuwapeleka watu katika sayari hiyo.
 
Tabia yako ya kulala inaratibiwa na aina ya Proteini inayoitwa PER. Kama utakuwa unafuata utaratibu mzuri wa kulala' kabla ya muda ambao huwa unakawaida ya kulala au kuamka' hujafika kiwango cha hiyo Proteini huzalishwa kwa wingi kwaajili ya kuandaa mwili kulala au Kuamka'.
 
Saudi Arabia' hakuna mto hata mmoja wala maji yanayotiririka, lakini watu wake katika mikoa yote wanapata maji safi na salama' kwaajili ya kunywa na kilimo'. Chanzo cha maji kwao ni chini ya ardhi na maji chumvi ya bahari ambayo huchujwa kuondolewa chumvi kisha hutumiwa na wananchi.
 
Mwaka 2014 mtu mmoja kutoka Hail, Saudi Arabia ambae hakutaka jina lake kutajwa aliweka Friji kubwa nje kwaajili ya watu mbalimbali kuweka vyakula kwaajili ya kuwasaidia watu maskini ambao hawajiwezi. Lengo ni kuwaondolea aibu ya kuomba chakula kwa watu badala yake kupitia Friji hizo mtu anachukua chakula bure bila kuomba.
 
Kuumia moyoni siyo msemo tu, ni ugonjwa unaosababishwa na maumivu ya kihisia. Kitaalamu unaitwa Heart Broken Syndrome. Na unaweza kupelekea hatari ya kupata magonjwa mengine hatari zaidi ya moyo. (WebMD, Heart Org, MayoClinic)
 
Uume' kwa asilimia fulani unajiongoza wenyewe bila uratibu wa akili (Ubongo). Ndio maana kuna wakati unasimama (erect) bila ubongo kuamrisha. Sababu nyingine ni Uume' umeundwa na baadhi ya Neva ambazo hazihitaji amri ya ubongo kufanya kazi, Neva hizo ndizo zinafanya kazi katika Moyo pia.
 
Kwa mwanaume kuamka asubuhi huku uume' ukiwa umesimama (Erect) ni kiashiria cha afya njema hususani katika njia zako za uzazi. Sababu mojawapo ni asubuhi kiwango cha homoni ya Testestorone' inakuwa kwa kiasi kikubwa hivyo hupelekea uume kusimama bila hiyari.
 
Dunia kujizungusha katika mhimili wake unakamilika kwa saa 23 dakika 56 na sekunde 4 na sio saa 24. Tafsiri ya siku kuwa na saa 24 sababu tunaangalia kuchomoza na kuzama kwa Jua muda unaochukua ndiyo hutimia masaa 24 (Dakika 4 zinazobaki hukamilika na kuwa saa 24).
 
Fisi (Spotted Hyena) hutoa sauti mfanano kama kicheko lakini sio kweli kwamba hucheka kama tafsiri ya wengi. Ukimuona anatoa namna hiyo ya sauti huwa ni ishara ya kuwaambia wenzake kuwa kaona windo, yupo eneo la hatari au yupo kwenye mpambano wa kupora chakula
 
Back
Top Bottom