Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Niko jeshi mwaka wa 10 nishindwe kuchinja kuku😎
Umenikumbusha miaka ya zamani bado hujazaliwa kulikua na nchi inaitwa Tanganyika, utaratibu wake ulikuwa ukihitimu masomo ngazi ya juu lazima uende jeshini kupatakuwa Jasiri na Mzalendo kitu ambacho sikukubaliana nacho nikaingia mitini...

Baada ya mafunzo kuisha nilikutana na jamaa yangu aliyetoka jeshini sasa wakati wa maongezi alidondokewa na Mjusi, sasa kelele alizopiga na kule kujirusha rusha ilikua ni vichekesho...

Samahani kwa hadithi ndefu ila nia ni kukuambia Jeshi halikupi uhakika wa kufanya hayo. Wacha tu kumchinja kuku wewe ata kumbeba huwezi
 
Kuna siku nilipewa adhabu ya kuchinja dume la ng'ombe duh ilikuwa kasheshe....

(Anyway hii ni nje ya mada yenu[emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099])
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…