Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
4.Zlatan Ibrahimovic Italy ni miongoni mwa nchi amabzo zimeathirika kwa kiasi kikubwa na virusi hivi hatari vya Corona, takwimu zinaonesha zaidi ya Waitaliano 4,032 wameshapoteza maisha kutokana na Corona.Kutokana na hali hiyo, Zlatan Ibrahim Movich, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram alimbulisha kampeni maalumu inayojulikana kwa jina la kimbiza virusi (kick away the Virus), ikiwa na lengo la kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia juhudi za kumbana na ugonjwa utokanao na virusi hivyo, katika Hospitali zilizopo Miji ya Milan, Rozzano, Turin na Bergamo.Taarifa kutoka mtandao ambao unatumika kuendesha kampeni hiyo zinasema kuwa, Zlatan alichangia kiasi cha Euro 100,000 na baada ya muda kiasi cha Euro 10,300 zilichagiwa na watu wengine.