Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waafrika tumekuwa hatupendi kujisomea hata vibandiko vidogo vidogo tu, tunasubiri asome mmoja ndio atusimulie,hapo ndipo upotoshwaji unapo anzia. Imefikia hatua hata kuziwaza shida zetu na namna ya kuzitatua tunaona uvivu. Tumebaki na midomo ya lawama hata kwa mambo ya kutatuliwa kifamilia inaangushiwa serikali.


Sent using Jamii Forums mobile app
Leo mnashusha nondo za kufa mtu wallahi....

Lakini pia na mifumo yetu ya elimu ni ya hovyo mno jamani. Haitufunzi kufikiri bali kukariri tu ili tupasi mitihani tupate ajira. Na Nyambari Nyangwine na vitabu vyake vya majibu ya mitihani ndiye mkombozi wetu. Tabia ya kufikiri na kuchambua mambo kwa kina itatoka wapi?

Fikiria hii ishu ya chanjo. Ebola tumekaa nayo tangu miaka ya 70 huko. Hakuna tulichofanya. Mwaka juzi hapa ikajichanganya ikavuka na kuingia Ulaya na Marekani. Wenyewe wakajikunja chini ya miaka miwili wakapata chanjo. Tukalia ubaguzi. Ooooh chanjo walikuwa nayo miaka na miaka hawakutaka kutupa sababu ya ubaguzi. Corona imeingia. Wanataka kutushirikisha kwenye parallel testing. Bado tunalia ubaguzi. Madawa ya Malaria wakitengeneza napo tunalia ubaguzi. Oooh madawa yana side effects mbaya. Yanatumalizia nguvu za kiume. Hawataki tuzaane. Kulalamika tu lakini hatufanyi cho chote. Ni kweli bara zima hili hatuna wataalamu na pesa za kufanyia tafiti na kutengeneza madawa na chanjo zetu wenyewe? Sisi ni ombaomba matajiri. Ombaomba waliodeka. Ombaomba wanaolia kuonewa na kubaguliwa. Ombaomba wa kujitakia. Watoto wa kambo (msemo wa KD). Spoiled brats !!!
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Yegomasika ana matatizo sana

Wiki iliyopita nilipita kule...


Sent using Jamii Forums mobile app
Eti mgumu lakini ukimuona na mazagazaga yake ya shughuli (maua, mvinyo, magauni, viatu...) mpaka unamuonea huruma. Hovyo kabisa...

Niliona. Nitakuja....[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Waafrika tumekuwa hatupendi kujisomea hata vibandiko vidogo vidogo tu, tunasubiri asome mmoja ndio atusimulie,hapo ndipo upotoshwaji unapo anzia. Imefikia hatua hata kuziwaza shida zetu na namna ya kuzitatua tunaona uvivu. Tumebaki na midomo ya lawama hata kwa mambo ya kutatuliwa kifamilia inaangushiwa serikali.


Sent using Jamii Forums mobile app

Binafsi naichukia sana Dunia ya lawama, Jamii zilizoendelea wameshaacha kabisa mambo ya lawama badala yake wamejikita kwenye uwajibikaji
 
Angalau wangeleta huu ufafanuzi tungewaelewa.
Kikubwa aliyepokea hiyo taarifa alipaswa kufafanua pia
Nimekuelewa sana.
Msikubali nini?

Waafrika nasi tumezidi kulalamika. Kama hatutaki si tutengeneze madawa yetu? Bara zima kila kitu tunategemea wazungu....

Hili suala liko hivi kisayansi: Vaccine inapofanyiwa majaribio, inabidi ifanyiwe katika population mbalimbali katika mazingira tofauti ili kuona kama kweli inafanya kazi kila mahali. Hutaki uingie gharama ya mabilioni kutengeneza chanjo/dawa ambayo inafanya kazi nusu nusu. Walichosema hao watengeneza chanjo hii ni kwamba wanataka kufanya parallel trials. Wameanzia kule Australia, Marekani, Ufaransa na wanataka pia nchi moja au mbili Afrika.

Afrika, kama inavyojulikana, hakuna huduma za kiafya za kueleweka. Hata kinga za kawaida tu ni shida. Kama chanjo hii itaweza kufanya kazi vizuri na kuzuia maambukizi kabisa hata katika mazingira haya, basi huu utakuwa ni uthibitisho tosha kwamba ni chanjo nzuri.

Sasa sisi Waafrika kila kitu tunafikiri ni ubaguzi na tunaongea sana na kujifanya tunajua kila kitu. Wakiacha tena halafu mambo yaje yafumuke huku na chanjo iwe haifanyi kazi sawasawa katika mazingira yetu kwa sababu tulikataa wakati wa testing napo yatakuwa maneno. Wazungu hawajali Waafrika hata tukifa na walitengeneza chanjo kwa ajili yao pekee.

Kama hatutaki tafiti za hawa jamaa basi tuamke tuanze kufanya za kwetu. Kongea tu na kulalamika kuwa tunabaguliwa haitatusaidia kwa lolote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2.27899907681509606E18.jpg
 
Back
Top Bottom