Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1586537708789.jpeg
 
Geoffrey Kondogbia, wa Valencia anayelengwa na Tottenham ambaye mkataba wake ni euro milioni 80 (£70.1m) huenda akahamia kwengine kwa kiasi cha chini, ikiwa klabu ya Uhispania ya kiungo huyo wa kati, 27, itashindwa kuingia katika ligi ya Champions msimu ujao. (Evening Standard)
 
Spurs huenda ikawa miongoni mwa wanaowania kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona, Philippe Coutinho. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 pia anapaniwa na Chelsea, ambayo ilikuwa inamtaka mchezaji huyo wa Brazil kwa mkopo lakini hilo kidogo wamelinyamazia kwasababu Barca inataka kuongeza kipengele ambacho baadae uhamisho huo utakuwa wa kudumu. (Mirror)
 
Manchester United bado inatafakari iwapo itampa mchezaji wa Nigeria Odion Ighalo, 30, mkataba wa muda mrefu wakati ambapo kocha Ole Gunnar Solskjaer bado hajaamua kuhusu kumsajili mshambulizi mwengine msimu ujao. Ighalo yuko kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua hadi mwisho wa msimu. (Evening Standard)
 
Matarajio ya Chris Smalling kupata uhamisho wa kudumu hadi Roma kutoka Manchester United yamepata pigo. Mchezaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 kwa kiasi kikubwa ameamua kusalia Italia ambako amekuwa kwa mkopo tangu mwishoni mwa Agosti. (The Sun)
 
Manchester United na Liverpool wako tayari kushindania usajili wa kiungo wa kati wa Aston Villa Carney Chukwuemeka. Mchezaji huyo, 16, wa timu ya Under-17 anakadiriwa kuwa mchezaji mzuri zaidi miongoni mwa vijana nchini humo. (The Sun via Athletic)
 
Back
Top Bottom