Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Amua ikiwa Unataka Kuuza Kwa Haraka au La!Watu wengi hawajui kuwa muda una nafasi kubwa katika mchakato wa kuuza fanicha iliyotumika. Ikiwa unahitaji kuuza fanicha yako kwa haraka, inashauriwa kupunguza bei ya bidhaa yako. Hii inaongeza nafasi za kuuza fanicha yako kwa haraka. Kwa nini? Mara zote watu wanatafuta bei rahisi.
 
Jifunze Jinsi ya Kujadili BeiKwa kawaida, wakati wa kuuza mtafikia muda wa kujadiliana bei na mnunuzi wa fanicha unayouza. Wewe unataka upate bei nzuri kwenye fanicha yako na wakati huo huo mnunuzi nae anataka anunue kitu cha bei rahisi. Wote mnakuwa kwenye hali mbili tofauti kabisa, lakini mara zote kuna mahali pa mkutano: mahali ambapo wot mnapata thamani katika ununuzi huo.
 
Usisite kuhusu kutaja bei yako hata kama muuzaji atataja bei ya chini sana. Kama tulivyoona hapo juu, muuzaji unaweza kutaja bei kwa kuangalia uhitaji wake wa pesa. Kama unadhani bei aliotaja ni ndogo sana kukupa faida au kufikia bei uliyoiweka. Lakini pia kama huna muda mwingi, basi usisite kumfanya apande dau na kama hatafika basi angalau awe ameikaribia. Wakati mwingine bei hiyo inaweza kuwa bora ukilinganisha na gharama za kurekebisha, kusafirisha au kupotea ikiwa utaamua kuiacha iendelee kuozea ndani.
 
Kuwa Muwazi Juu ya Uzima wa Fanicha YakoNi kawaida kwa fanicha kupata uharibifu kidogo wakati wa matumizi. Wewe unalijua hili na wanunuzi wanalijua pia. Kuwa mkweli na toa maelezo ya kutosha ukiambatanisha picha za fanicha zioneshazo mikwaruzo, michaniko, sehemu uliyorekebisha n.k.
 
Wanunuzi wanapenda kujua wananunua nini mapema. Wengi huwa hawajali kuhusiana na uharibifu mdogo (ili mradi uendane na thamani) na ni bora tu wajue mapema. Kumbuka kwamba soko la bidhaa zilizotumika linategemea kuaminiana. Mnunuzi kumuamini muuzaji na hii ndio inayowahimiza watu kununua vitu vilivyotumika kwa mtu ambaye hawajawahi kukutana naye.
 
Unahitaji kuwafanya wateja wako wawe na furaha. Unahitaji kuwafanya wawe wateja wanaokuja kwako kila mara na waweze kuleta marafiki zao. Kama utakuwa na wateja wasio na furaha, wanaweza wakasambaza maneno ya sio mazuri kuhusu biashara yako kwa watu wengine.
 
Wakati wa kuchunguza kuhusu soko, unatakiwa kutafuta kujua juu ya mahitaji, matakwa, maslahi na idai ya wateja wako. Ukijua wanachotaka, utaweza kuwapa. Mfano, kama umetafiti na kugundua sehemu fulani kuna uhaba wa viatu vya ngozi, ni rahisi kuanzisha biahsara hivyo na kupata watu. Wateja wakipata wanachotaka, lazima wafurahi, lazima wathamini biashara yako.
 
Back
Top Bottom