Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Njia ya pili ni kula embe lililomenywa. Yaani unaondoa maganda na kuikata vipande na kula nyama yake. Ulaji wa namna hii unatumiwa na watu wengi. Hata hivyo, virutubisho vingi vinavyopatikana kwenye maganda ya embe kama vile nyuzilishe, madini, vitamini na “phytochemicals” vinapotea wakati wa umenyaji.
 
Njia ya tatu, ni kula embe na maganda yake. Ulaji wa aina hii ni mzuri hasa kwa watu ambao sio wagonjwa. Ulaji huu unaupa mwili virutubisho vingi zaidi vilivyomo kwenye nyama na maganda ya embe husika. Hata hivyo, kabla ya kula lazima embe lioshwe vizuri na lisuuzwe kwa maji safi na salama; yaliyochemshwa au ya chupa. Baada ya hapo ndipo liliwe na maganda yake.
 
Kama embe halitaoshwa vizuri, mlaji anaweza kupata maambukizi ya magonjwa kama vile kipindupindu, homa ya matumbo, kuhara na minyoo. Kwa yale yanayopuliziwa dawa za kuua wadudu, yakiliwa bila ya kuoshwa vizuri dawa hizo zinaweza kudhuru afya ya walaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…