HBD
Kivuruge wa watu....
View attachment 1431252
Utani pembeni naomba niseme tu kwamba wewe u dada na binadamu mwema sana. Nilipofiwa na mama ulisimama kidete ukanisaidia sana bila kuchoka. Nikiwa mpweke halafu mbali na nyumbani, ulikuwa nguzo imara ambayo kwayo niliweza kuegemeza kichwa changu nikalia bila kuogopa. Mpaka leo huwa nasoma ushauri wako na kulengwa lengwa na machozi. Naamini Mungu Alikutumia kipindi kile ili kupunguza maumivu yangu; na uliutii wito huo kwa unyenyekevu sana.
Kwangu ulipanda mbegu za wema, unyoofu wa moyo na ubinadamu ambazo daima zitaendelea kuchipuka.
Na mimi nikitendewa wema huwa sisahau kamwe. Hunijui sikujui lakini natumaini siku moja nitaweza angalau kukushukuru kwa uhalisia zaidi.
Nakuombea Mungu Akupe maisha marefu yenye amani, furaha na ridhiko tele. Wema wako ulionionyesha wakati ule nami nitauendeleza kwa wengine huko. I will pass it forward...and that's how we make our world a better place. Barikiwa sana shemeji na Mungu Akulinde uvuke salama katika mapambano haya ya Korona. You are a blessing to many mbali na ukivuruge wako sometimes...[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
View attachment 1431253