Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Adjustments.JPG
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
[emoji267][emoji268][emoji271][emoji269]CARBAMAZEPINE [emoji269][emoji271][emoji268][emoji267]

Binti yangu mpole,faraja yangu,kivuruge wangu, ukaribu wako kwangu kwa kila anguko linitokeapo unanifanya niwe imara zaidi.
Ukinipigia simu nikikuitikia "mamaangu..." kama kuna tatizo unagundua mara moja cha upole wangu... "baba ni nini tena?... "

Sikupati hewani lakini naamini hapa utaonekana maana ndio makazi yetu ya furaha na amani tujumuikapo wana familia.
Ahsanteni wana uzi huu kwa kumfanya binti yangu angalau aweze hata kuongea na watu, upole wake ulikuwa unatia hofu...

Binti yangu carbamazepine nakuombea maisha marefu yenye furaha na amani tele sawa sawa na mapenzi ya Mungu,kila jambo lako likapate kutimia kwa wakati[emoji120][emoji120]

Happy birthday kivuruge

Umesha kuwa mkubwa sasa...
#siolazimauolewenatakawajukuu
View attachment 1431229

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HBD Kivuruge wa watu....

View attachment 1431252

Utani pembeni naomba niseme tu kwamba wewe u dada na binadamu mwema sana. Nilipofiwa na mama ulisimama kidete ukanisaidia sana bila kuchoka. Nikiwa mpweke halafu mbali na nyumbani, ulikuwa nguzo imara ambayo kwayo niliweza kuegemeza kichwa changu nikalia bila kuogopa. Mpaka leo huwa nasoma ushauri wako na kulengwa lengwa na machozi. Naamini Mungu Alikutumia kipindi kile ili kupunguza maumivu yangu; na uliutii wito huo kwa unyenyekevu sana.

Kwangu ulipanda mbegu za wema, unyoofu wa moyo na ubinadamu ambazo daima zitaendelea kuchipuka. Na mimi nikitendewa wema huwa sisahau kamwe. Hunijui sikujui lakini natumaini siku moja nitaweza angalau kukushukuru kwa uhalisia zaidi.

Nakuombea Mungu Akupe maisha marefu yenye amani, furaha na ridhiko tele. Wema wako ulionionyesha wakati ule nami nitauendeleza kwa wengine huko. I will pass it forward...and that's how we make our world a better place. Barikiwa sana shemeji na Mungu Akulinde uvuke salama katika mapambano haya ya Korona. You are a blessing to many mbali na ukivuruge wako sometimes...[emoji1545][emoji1545][emoji1545]

View attachment 1431253
Aisee, pole sana bro.
Sikuwahi kuipata hii habari.

Natumai ni kwema huko.
 
Back
Top Bottom