“Nina uhakika bado tuna nafasi ya kuwa mabingwa. Itakuwa mbaya sana kama msimu utafutwa. Na hilo likitokea, basi itakuwa sio haki kabisa kwa Barcelona kupewa ubingwa. Wao Barcelona wataona sawa, lakini sitawaelewa kabisa,” alisema.
“Wametoka sare na kufungwa na sisi, tuliwaonyesha kwamba sisi tupo vizuri hata kama wao wapo juu kwa pointi mbili zaidi yetu. Inakuwa sio haki. Kule England ningeweza kuwaelewa Liverpool wakitangazwa mabingwa kwa sababu wanaoongoza kwa tofauti ya pointi 25. Iwe tutacheza msimu wote umalizike au usimalizike, wataendelea kuwa mabingwa.”
Kipa Courtois amethibitisha kwamba atafanyiwa vipimo vya corona ikiwa ni mpango wa La Liga kufahamu ukubwa wa tatizo hilo kwa wachezaji kabla ya kuamuru ligi kuendelea. Mpango wa La Liga ni kuendelea na ligi mwezi ujao bila ya mashabiki uwanjani kama inavyopangwa kutokea kwenye Ligi Kuu England na Serie A (Italia).
Hispania imelegeza masharti ya kujifungia ndani baada ya kutokea vifo 25,000 kutoka kwa watu 250,561 walioambukizwa virusi vya corona huku maambukizi na vifo vikipungua kila siku.
Arsenal ilimnasa Pepe kutoka Lille kwa mkwanja mrefu, wakivunja rekodi yao ya uhamisho walipomnasa kwa Pauni 72 katika dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana.
Lakini, miamba hiyo ya Emirates ilikubaliana na Lille kuwalipa pesa hiyo kwa awamu na sasa mambo yanakuwa magumu baada ya sakata la corona ambalo limezitikisa timu nyingi za Ulaya kiuchumi.
NYOTA wa zamani wa Chelsea, Solomon Kalou ameiomba radhi klabu yake ya Hertha Berlin, baada ya kugundulika alivunja kanuni ya kuepuka mikusanyiko dhidi ya wachezaji wenzake katika kipindi hiki cha kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona.
Kalou alichapisha kipande cha video katika ukurasa wake wa Facebook, ambayo ilimuonesha akivunja kanuni hiyo ya kuepuka mikusanyiko, baada ya kumshika mkono mchezaji mwenzake wakati wanafanyiwa vipimo, video ambayo hata hivyo ameifuta.
Timu yake Hertha Berlin ya Ujerumani, imeamua kumchukulia hatua za kinidhamu kwa kumsimamisha mchezaji huyo raia wa Ivory Coast, kutohudhuria mazoezi na mwendelezo wa baadhi ya michezo ya Bundasliga.
Mkurugenzi wa michezo na mawasiliano wa klabu hiyo Michael Preetz, kitendo hicho cha Kalou sio tu kinatoa taswira mbaya kwa timu hiyo, bali hata kwa baadhi ya wachezaji mmoja mmoja wanaonesha hawana umakini katika kukabiliana na virusi vya corona.
Baada ya kupigwa rungu hizo, Kalou ameonesha kuwa hakukusudia kufanya hivyo, ambapo ameamua kuomba radhi kwa kitendo hicho na kwamba alifanya kwa furaha, baada ya majibu ya vipimo kuwa mazuri.
"Samahani kama nilionesha kutochukulia corona kwa umakini mkubwa, bali nilifanya vile kuonesha furaha ya vipimo vyetu kuwa vilikuwa hasi"- amesema Kalou.
Kabla ya janga la corona, Arsenal walikuwa na uhakika wa kuwa na pesa ya kulipa deni hilo huko Lille huku wakiwa na mkwanja mwingine wa kufanya usajili wa wachezaji wengine kadhaa kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi.
Lakini, sasa kwa mujibu wa Bleacher Report, mabosi wa Arsenal wanafirikia kuwaweka sokoni baadhi ya wachezaji ili kutoingia kwenye matatizo na Lille katika kumalizia pesa za usajili wa Pepe.
Wachezaji kadhaa kwenye kikosi cha kanza cha Arsenal akiwamo straika Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye mwisho wa msimu atakuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, anahusishwa na mpango wa kuachana na timu hiyo.
Licha ya Pepe amekuwa na mwanzo wenye mapito mengi huko Arsenal, staa huyo wa Ivory Coast amefunga mabao sita na kuasisti mara nane kwenye Ligi Kuu Englnd na Europa League.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.