Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

“Nina uhakika bado tuna nafasi ya kuwa mabingwa. Itakuwa mbaya sana kama msimu utafutwa. Na hilo likitokea, basi itakuwa sio haki kabisa kwa Barcelona kupewa ubingwa. Wao Barcelona wataona sawa, lakini sitawaelewa kabisa,” alisema.
 
“Wametoka sare na kufungwa na sisi, tuliwaonyesha kwamba sisi tupo vizuri hata kama wao wapo juu kwa pointi mbili zaidi yetu. Inakuwa sio haki. Kule England ningeweza kuwaelewa Liverpool wakitangazwa mabingwa kwa sababu wanaoongoza kwa tofauti ya pointi 25. Iwe tutacheza msimu wote umalizike au usimalizike, wataendelea kuwa mabingwa.”
 
Kipa Courtois amethibitisha kwamba atafanyiwa vipimo vya corona ikiwa ni mpango wa La Liga kufahamu ukubwa wa tatizo hilo kwa wachezaji kabla ya kuamuru ligi kuendelea. Mpango wa La Liga ni kuendelea na ligi mwezi ujao bila ya mashabiki uwanjani kama inavyopangwa kutokea kwenye Ligi Kuu England na Serie A (Italia).
 
NYOTA wa zamani wa Chelsea, Solomon Kalou ameiomba radhi klabu yake ya Hertha Berlin, baada ya kugundulika alivunja kanuni ya kuepuka mikusanyiko dhidi ya wachezaji wenzake katika kipindi hiki cha kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona.
 
Kalou alichapisha kipande cha video katika ukurasa wake wa Facebook, ambayo ilimuonesha akivunja kanuni hiyo ya kuepuka mikusanyiko, baada ya kumshika mkono mchezaji mwenzake wakati wanafanyiwa vipimo, video ambayo hata hivyo ameifuta.
 
Mkurugenzi wa michezo na mawasiliano wa klabu hiyo Michael Preetz, kitendo hicho cha Kalou sio tu kinatoa taswira mbaya kwa timu hiyo, bali hata kwa baadhi ya wachezaji mmoja mmoja wanaonesha hawana umakini katika kukabiliana na virusi vya corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…