Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatua ya Kwanza – Stage N1
Unapoingia kutoka kuwa macho hadi usingizi tulivu, unatumia kiasi cha dakika tano kwenye hatua ya kwanza -stage N1. Katika hatua hii, joto la mwili huanza kuteremka, misuli hulegea na macho hucheza taratibu kutoka upande mmoja hadi mwingine. Katika hatua hii, utapoteza ufahamu wa mazingira, lakini unaweza kuamshwa kirahisi.
 
Hatua ya Tatu – Stage N3
Katika hatua hii mwili wako unaingia kwenye usingizi mzito. Upumuaji unakuwa na mpangilio zaidi. Msukumo wa damu huteremka na mapigo ya moyo kuteremka kwa asilimia 20 hadi 30. Ubongo hupunguza usikivu wa vitu vya nje na kufanya kazi ya kumwamsha aliyesinzia kuwa ngumu zaidi.
 
Mtiririko wa damu kuelekea kwenye ubongo hupungua, na ubongo hupoa kwa kiwango kikubwa. Mwanzoni kabisa mwa hatua hii, tezi ya pitutary hutoa homoni za ujenzi wa mwili ambayo itaamsha ujenzi wa tishu na ukarabati wa misuli. Utafiti umegundua kuongeka kwa damu yenye vitu vya kuamsha kinga za mwili, kuongeza uwezekano wa kuwa mwili hujikinga dhidi ya maambukizi ya wadudu.
 
Ni mara chache sana watu wa umri wa zaidi ya miaka 65 kupata usingizi mzito. Ukilala baada ya kipindi cha kukosa usingizi, utapitia kwa haraka hatua za usingizi tulivu na kuingia hadi hatua ya usingizi mzito na kutumia muda mwingi pale. Hii inaashiria kuwa usingizi mzito una nafasi kubwa sana katika kurudisha umakini wa mwili na kuuweka mwili kwenye hali bora.
 
Ubongo unapo kazini, ukifikiri na kuota ndoto, wakati huo macho yakichezaka ndani ya kope zilizojifunga. Joto la mwili hupanda, pressure huja juu, mapigo ya moyo hupanda na upumuaji huwa ni wa haraka kama wa mchana. Wakati huu mwili hauna mwondoko wo wote, misuli isiyohitajika katika kupumua hutulia.
 
Utafiti umeoonyesha kuwa mwanafunzi aliyepewa kazi ya kutoa majibu kwa swali linalohusu umbo gumu lisiloeleweka, akapewa nafasi ya kulala usiku mmoja, anakuwa na nafasi ya kutoa majibu mazuri zaidi kuliko yule aliyepewa swali hilo hilo kwa kushtukiziwa na kutakiwa kutoa majibu.
 
Utafiti wa zamani unaonyesha kuwa usingizi wa ndoto husaidia kujifunza na kumbukumbu. Watu waliotahiniwa kuona jinsi walivyolielewa jambo geni, walionyesha kufanya vizuri zaidi baada ya kupewa usiku mmoja wa kupumzika. Wangeamshwa kila mara wanapoingia kwenye usingizi wa ndoto, mwongezeko huu wa ufaulu ungepotea.
 
Kwa upande mwingine, wangeamshwa kila walipoingia kwenye usingizi tulivu, hakungetokea mabadiliko katika mwongezeko wa ufaulu wao. Hii inaeleza kwa namna moja kwa nini wanafunzi wanaokesha na kukariri kwa ajili ya mtihani hawafanyi vizuri ukilinganisha na wale waaliopata usingizi.
 
Back
Top Bottom