Newcastle wako tayari kutumia £53m kumpata mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale, 30, mpango ambao ukifanikiwa utamrejesha ntota huyo katika ligi kuu ya England msimu huu. (Daily Mail)
Tottenham haitakubali Tanguy Ndombele, 23, kuondoka klabu hiyo msimu huu. Kiungo huyo wa kati wa Mfaransa amehusishwa na tetesi za kujiunga na Barcelona na Liverpool. (Independent)
Dejan Lovren anakaribia kuondoka Liverpool, huku Roma ikitarajiwa kuwasilisha ofa ya kumnunua beki huyo wa Croatia wa miaka 30. (Gazzetta dello Sport, via Liverpool Echo)
Liverpool imeungana na miamba wengine wa Ulaya kumsaka kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai,19. (Tuttosport, via Daily Mail)
Manchester United wanataka kuwasajili wachezaji watatu wa Uingereza msimu huu akiwamo- mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na kiungo wa kati wa Birmingham wa miaka 16, Jude Bellingham. (Daily Star)
Hata hivyo huenda, mshambuliaji Odion Ighalo, 30, akacheza mechi yake ya mwisho Manchester United maa ya mazungumzo ya kurefusha mkataba wa mkopo wa kiungo huyo wa kimataifa wa Nigeria kutoka Shanghai Shenhua nchini China kugonga mwamba. (Standard)
Juventus wamekuwa klabu ya kwanza ya Italia kuweka kanuni ya mshahara kwa wachezaji wake, hatua ambayo imewafanya kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba,27 . (Daily Mail)
Lionel Messi, 32, na baadhi ya wachezaji wenzake nchini Uhispania huenda wakapunguziwa mshahara kwa asilimia 30 msimu ujao huku Barcelona na Real Madrid wakitathmini hatua ya kupunguza marupurupu ya wachezaji kutokana na athari iliyosababishwa na virusi vya corona. (Sun)
West Brom itachuana na Tottenham kumsajili mshambuliaji wa Fenerbahce na Kosovo Vedat Muriqi, 26, mwenye thamani ya £uro milioni 18 iwapo atafanikiwa kupanda daraja. (Aksam, via Birmingham Mail)
KLABU sita zinazoshika nafasi za chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu England zimedai kwamba hazitagomea kuendelea na ligi kama tu suala la kushushwa daraja halitakuwapo msimu huu.
Norwich, Watford, Aston Villa, Bournemouth, West Ham na Brighton zipo tayari kushawishi timu nyingine kuendelea na ligi hadi imalizike kwa kucheza pia kwenye viwanja huru.
Lakini, watafanya hivyo kama tu suala la kushuka daraja litaondolewa wakati itakapojadiliwa kuhusu kuendelea na msimu hadi mwisho katika kikao kitakachofanyika Jumatatu
Ofisa mmoja wa ngazi za juu kutoka kwenye moja ya klabu hizo alisema: “Kila mtu anajaribu kuvutia upande wake, lakini hii ishu ya kuondoa faida ya kucheza nyumbani si kitu kinachoweza kujadiliwa kirahisi hasa kwa timu zilizopo kwenye hatari ya kushuka daraja.”
Hicho ni moja ya vikwazo vingi ambavyo chama cha soka kinapaswa kuweka mambo sawa linapokuja suala la kushuka daraja. Klabu zinaonekana kugomea kucheza mechi kwenye viwanja huru.
Mjadala umekuwa mzito na kwamba hata kama klabu zitakubaliana pamoja na kampuni ya televisheni, lakini shida nyingine inaweza kutokea kwa wachezaji kwa sababu si wote wanaounga mkono ligi hiyo kuendelea
Winga wa Brighton, Anthony Knockaert alisema: “Ujerumani wataanza ligi yake hivi karibuni na hilo halikubaliki, kwa sababu ni hatari sana kwa jamii na wachezaji. Sidhani kama ni uamuzi mzuri kuendelea kucheza katika hali kama hii, wachezaji watakuwa kwenye hatari kubwa sana.
“Nadhani wengi watakubaliana na mimi. Inatisha. Naogopa kupata virusi hata nikienda dukani tu, vipi kwenye mechi. Hata nikipata, mimi ni kijana na afya yangu ipo vipi. Vipi nikienda kuwaambukiza wengine ambao afya zao ni hatari zaidi
“Sote tuna familia zetu nyumbani. Nina miaka 28, nina watoto na familia nyingine ambayo nakwenda kuonana nayo mara kwa mara. Ni hatari sana hiki kitu kikitokea na kitaenda kubaki kwenye kumbukumbua kwa miaka mingi.“Nimeona ligi tatu zimesitishwa. Ubelgiji, Ufaransa na Uholanzi.“Kwangu hao wamefanya uamuzi mzuri.Subiri tuone nchi nyingine zitafanyaje. Jambo hili nadhani wachezaji nao wapewe nafasi ya kutoa maoni yao.”
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.