Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2. Uwezo wa kufanya maamuzi - Kufikia malengo yako itakubidi ujenge uwezo wa kufanya na kufikia maamuzi kwa haraka juu ya jambo lolote katika maisha yako na kuyabadili pale inapohitajika.Kuruhusu hali ya kushindwa kufanya maamuzi kwa sababu ya hofu ama kitu au mtu fulani ni kikwazo cha mafanikio yako.
 
3.Kuwa na mtazamo chanya juu ya maisha – Mtazamo sahihi katika maisha ni nguzo muhimu katika kufikia mafanikio yoyote. Amini kuwa kile ulichokikusudia inawezekana kukifikia na kuwa unao uwezo wa kufanikisha lengo hilo. Kujiamini juu ya uwezo wako ni nyenzo katika mafanikio.
 
4.Kuwa na nidhamu ya maisha – Nafsi ni rafiki mkubwa na pia ni adui mkubwa sana wa mtu. Bila kuwa makini na nafsi yako utajikuta unafanya mambo ambayo yako kinyume na malengo yako katika maisha. Uwezo wa kumudu matakwa ya muda mfupi ya nafsi ni jambo la kuzingatia ili kuhakikisha hautoki katika mstari wa kile ulichokusudia.
 
5.Kutokata tamaa – Watu walio wengi ni wazuri wa kuanzisha kitu lakini ni wachache wetu wanaoweza kufika hadi mwisho wa kile walichokianzisha. Wengi hujikuta wakikata tamaa baada ya kukutana na changamoto kadhaa. Kutokata tamaa ndio kitu pekee kitakacho kuwezesha kufikia yale uliyoyakusudia, haijalishi ni magumu yapi utapitia usikubali nia yako ya awali ipotee.
 
6.Kuchukua hatua leo – Watu wengi wanasubiri muda muafaka ufike ili waweze kuchukua hatua ya kutekeleza malengo yao. Usisubiri! Hakuna siku utaona kuwa leo ndio muda muafaka wa kutenda, anza na kile ulichonacho na mengine mengi utayapata mbale ya safari.
 
7.Kufanya uchaguzi sahihi wa marafiki na mwenzi wa maisha – Mwenzi wako anachukua sehemu kubwa katika maisha yako, ni suala la msingi kuchangua mwenzi sahihi anayeendana kitabia na kimtazamo na wewe. Uhusiano mbaya baina ya wawili unamfanya mtu kupoteza matumaini na motisha ya maisha na hivyo kujikuta akishindwa kufikia mafanikio aliyoyakusudia awali. Mtu ni matokeo ya watu wanaomzunguka, kuwa makini kuchagua marafiki ,wawe ni wale ambao watakutia nguvu na kukupa changamoto za kufikia malengo yako.
 
8.Utayari wa kujifunza – Dunia ya sasa iliyojaa utandawazi na teknolojia inahitaji mtu aliye tayari wakati wowote kujifunza ili kuweza kukabiliana na ushindani pamoja na mabadiliko yanayotokea kila siku. Kujifunza si lazima uende darasani bali kuna njia nyingi sana za kujifunza mambo mbalimbali katika maisha.
 
9. Afya njema – Hauwezi kufanikisha jambo lolote kama afya yako ni ya mgogoro. Jitahidi wakati wowote afya yako iwe nzuri ili muda wote uwe na nguvu ya kufanya kazi kuweza kufanikisha malengo yako. Zingatia ushauri wa wataalamu wa afya kuweka mwili wako safi wakati wowote.
 
10. Kushirikiana na kujitoa kwa ajili ya wengine – Unapojitoa kwa ajili ya wengine ndipo unapata zaidi. Kila mtu ana uwezo wake na fursa mbalimbali katika mambo tofauti tofauti, ushirika mzuri na wengine utakuwezesha kupata baadhi ya fursa muhimu na msaada mzuri kutoka kwa wengine na hivyo kukusaidia kufanikisha mambo yako.
 
Sijambo binti yangu mwema. Za kupotea?

Anayekunyima uhuru wako huyo mwambie siku zake zinahesabika [emoji16][emoji16][emoji16]

Stay blessed binti mpole wewe [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Nzuri tuu dadiii

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ntamwambia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…