Hii Ni Orodha Ya Makabila Ya Tanzania.Kuna matatizo kwenye majina kadhaa katika orodha hii, kwasababu mbalimbali. Orodha hii inatokana na orodha ya Ethnologue ya lugha za Tanzania, pamoja na tovuti nyingine. Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya. Juu ya hivyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema kwamba kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vinavyo mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.