Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo. Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya Kilimanjaro Siha, Machame. Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu, Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo, Wa-Uru, na Wa-Siha.Lugha ya Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kimarangu, Ki-Old Moshi,Kikibosho, Kimachame, Kikirua na Kisiha. Lugha hizi zinakaribia kufanana kulingana na jinsi makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua, ambacho nacho kinafanana kidogo na Kimarangu. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
 
Majina ya Kichagga Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo. Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.
 
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.
 
Wagogo (mmojawao anaitwa Mgogo) ni kabila la Tanzania ya kati, wenyeji wa mikoa ya Dodoma na Singida. Lugha yao ni Cigogo (kwa Kiswahili hutamkika Kigogo).Dini ya wengi wao ni Ukristo, hasa wa madhehebu ya Anglikana, halafu wa Kanisa Katoliki. Historia ya Wagogo inaweza kuelezeka kwa kuangalia yafuatayo: Utawala wa jadi, nyumba za asili, chakula kikuu na lafudhi ya lugha. Majina ya ukoo ya Cigogomajina hayo ni kama Mazengo, Cidosa, Cilongani, Malecela, Mwaluko, Mavunde, Ndejembi, Manyesela, Mbogambi, Mdachi, Kapaya,Matonya, Mtunya, Kusila, Nhonya,Mhalanyuka, Mbenaa, Chibile, Mdoli, Lusinde,Njamasi,Majenda,Chiwamba,Mazoya,Ufinyu,Chilyawanhu,Magaya, Ngoli,Chiwanga,Lubeleje,Makupila,Fukunyi
 
Back
Top Bottom