Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ancelotti pia anajaribu kumsajili Mbrazili anayekipiga St-Germain katika nafasi ya ulinzi Thiago Silva kwa uhamisho huru, mara tu mkataba wake utakapokwisha msimu huu. (Express).
 
Mustakabali wa Jadon Sancho kwenye kikosi cha Borussia Dortmund bado umekuwa si wa uhakika baada ya kocha mkuu Lucien Favre kumuorodhesha mshambuliaji huyo,20, kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza kuondoka msimu huu. (Sky Sports)
 
Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann amesisitiza kuwa Timo Werner, 24, bado yuko kwenye mipango ya timu hiyo kwa ajili ya ligi ya Champions, ingawa mshambuliaji huyo amekubaliana na Chelsea. (Mirror)
 
Chelsea imeongezewa nguvu katika mbio zake za kumnasa Kai Havertz huku Bayern Leverkunsen ikisema hawata 'mzuia' iwapo atataka kuondoka baada ya kiungo huyo Mjerumani, 21 kusema anahitaji changamoto mpya. (Kolner Stadt-Anzeiger-in German)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…