Gusa kitu mara moja na malizana nacho. Muda umekuwa tatizo kwa wengi kwa sababu hawana mpangilio mzuri. Jiwekee sera ya kugusa kitu mara moja na kuachana nacho, hasa kwenye mawasiliano. Mfano kama umetenga muda wa kusoma email, kila email unayofungua isome na kuchukua hatua hapo hapo, usijiambie naihifadhi nije kuifanyia kazi baadaye, hapo unapoteza muda. Hivyo pia kwenye barua na kazi nyingine unazofanya, gusa mara moja na malizana nacho.