Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mipango yako binafsi ya baadaye inapaswa kuwa siri yako. Kwenye kazi, kama una mpango wa kuja kuacha kazi hiyo siku za mbeleni, hilo linapaswa kuwa siri yako na mtu yeyote asijue. Kwa sababu inapotokea changamoto na watu wakahitaji kupunguzwa, utaanza kupunguzwa wewe ambaye umeshaonesha kwamba siku zijazo utakuja kuondoka, na hilo litaweza kuharibu mipango yako ya baadaye.
 
KUCHUKUA HATUA ZA HATARI.

Shindwa haraka na shindwa mapema. Chochote unachofanya kwenye kazi au biashara, hutaweza kufanikiwa kama unafanya kawaida. Unahitaji kuchukua hatua ambazo zinaonekana ni za hatari. Hivyo unahitaji kushindwa haraka na kushinda mapema, kwa kujaribu vitu hatari. Kwa kushindwa huko, utakuwa umejifunza mapema na kujua kilicho sahihi kufanya.
 
Tumia fedha za watu wengine. Unapotaka kukuza zaidi biashara yako, njia bora ni kutumia fedha za wengine. Na fedha nzuri kutumia ni kutafuta watu wa kuwekeza kwenye biashara yako. Mikopo siyo mizuri, hasa biashara inapokuwa changa. Lakini kuwa na wawekezaji kunakupa uhuru wa kukuza zaidi biashara yako.
 
Usiwekeze kwenye biashara ambayo waanzilishi wake wameshaondoka. Biashara huwa zinakua na kuwa na ubunifu pale ambapo waanzilishi wa biashara hizo wanakuwepo kwenye biashara hizo. Kwa sababu wao ndiyo wenye maono makubwa ya biashara hiyo. Wakishaondoka hao kinachobaki ni siasa tu, na kuangalia faida zaidi ya ukuaji. Kampuni nyingi huanza kuanguka pale waanzilishi wanapoondoka.
 
MBINU BORA ZA MAUZO.

Fanya vitu vichache kwa ufanisi mkubwa kuliko kufanya vitu vingi kwa ukawaida. Uza vitu vichache vyenye ubora wa juu badala ya kuuza vitu vingi vyenye ubora wa kawaida. Kwenye mauzo yako, sema maneno machache na muhimu.
 
Ongea kwa mapenzi na hamasa. Pale unapoongelea bidhaa au biashara yako, ongea kwa mapenzi na hamasa kubwa. Kadiri unavyopenda na kuhamasika na kile unachouza, ndivyo unavyoweza kuwashawishi wengine kukubaliana na wewe. Kama unaongea kwa kutokujiamini, kwa sauti ya chini na kukata tamaa, hutaweza kumuuzia mtu yeyote.
 
Ukishajua mtu anataka kununua kitu, kaa kimya. Wakati wa kumshawishi mtu kununua kitu, wauzaji wengi hujikuta wanaongea sana mpaka mtu anaahirisha kununua kitu. Ondokana na hilo kwa kuongea maneno machache na muhimu, na pale mtu anapoonesha nia ya kununua, kaa kimya, usiendelee kuongea tena. Hapo mtu atafanya maamuzi na kununua.
 
Wateja wadogo wanahitaji kazi kuliko wateja wakubwa. Kwenye biashara yako, chagua kuwahudumia wateja wakubwa na utaweza kufanikiwa zaidi. Ukikazana kukimbizana na wateja wadogo, watakupa kazi kubwa sana. Kwanza watataka punguzo kwa sababu bajeti yao ni ndogo na pili watahitaji sana msaada wako hata baada ya kununua. Wateja wakubwa wanakuwa na bajeti kubwa na wana timu ya watu wa kufanyia kazi vitu hivyo hawatakutegemea sana wewe.
 
Usisikie neno hapana. Unapowashawishi watu kununua kitu, watakuwa na mapingamizi mengi. Kama utayasikia mapingamizi hayo na kukubaliana nao, hutaweza kuuza kamwe. Wewe endelea kuwashawishi watu wanunue na kadiri unavyong’ang’ana ndivyo wanavyokuwa tayari kukubali.
 
Back
Top Bottom