Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JINSI YA KUVUKA SIASA ZA OFISINI.

Andika ujumbe na uhifadhi. Mtu anaweza kukuudhi kweli kweli, na ukamwandikia ujumbe, labda kwa siku, au email. Kabla hujatuma ujumbe huo, uhifadhi mpaka kesho yake, kisha njoo usome tena kabla hujautuma. Mara nyingi utajikuta siyo ujumbe sahihi kutuma. Somo ni usiwe unajibu unapokuwa na hasira, jipe muda wa kutulia na utaona hatua sahihi za kuchukua.
 
Dini na siasa ni aina mbili za mijadala unayopaswa kuiepuka sana eneo lako la kazi au biashara. Hii ni mijadala inayowagawa watu sana. Unaofanya biashara inayohusisha watu wa aina mbalimbali, usiweke wazi msimamo wako wa kidini au kisiasa, haitakusaidia chochote zaidi ya kukupunguzia wateja.
 
Kamwe usimseme mtu ambaye hayupo, kama mtu amekuja kwako na habari za mtu mwingine, mwambie subiri tumwite mtu huyo asikie unavyomsema. Na unapowakuta watu wanamsema mtu mwingine, sema kitu chanya kuhusu mtu huyo au ondoka hapo haraka. Chochote kibaya unachosema kuhusu wengine, jua kitawafikia.
 
Angalia wengine wanafanyaje kisha na wewe fanya kama wao. Unapoenda kwenye mazingira mapya ya kazi au biashara, haitasaidia kama utaonekana ni mtu wa tofauti kabisa. Jua utamaduni wa eneo husika kisha nenda nao. Kile unachofanya fanya kwa ubora kabisa, lakini usivunje utamaduni uliozoeleka.
 
Kwenye kazi kama unataka kupandishwa cheo, lazima uwe mtiifu kwa wale walio juu yako. Lazima uwe tayari kunyenyekea hata pale ambapo unaonewa kabisa. Wale wanyenyekevu na watiifu ndiyo wanapata nafasi za kupanda juu. Kama huwezi kunyenyekea hata pale wa juu yako anapokosea, basi ingia kwenye biashara, kwenye kazi itakuwa vigumu sana kwako kupanda juu.
 
Kwenye kazi, kadiri unavyoonekana ndivyo unavyochukuliwa kama mchapakazi. Hivyo ili kupata nafasi za kupanda vyeo kwenye kazi, hajalishi unafanya kazi kiasi gani, unatakiwa ujioneshe kwa watu sahihi pia kwamba unafanya kazi. Kwa kifupi maigizo yanahusika sana ili kupandishwa cheo kwenye kazi. Kama huwezi maigizo basi ingia kwenye biashara, kazi itakuwa ngumu sana kwako.
 
Usimwamini mtu yeyote. Kwenye kazi na biashara, kila mtu anaweza kuwa adui yako muda wowote ule, kwa sababu kila mtu anaangalia maslahi yake zaidi ya wengine. Hivyo mara zote kuwa makini, mara zote fanya kile kilicho sahihi na usimwamini mtu yeyote, kila mtu ana ajenda zake binafsi.
 
WENYE WASIWASI NDIYO WANAOPONA.

Wanasema wasiwasi akili, kuwa na wasiwasi ambao unakutaka uthibitishe kwanza kitu kabla ya kufikia maamuzi, unasaidia. Mfano kabla hujatuma ujumbe wowote, rudia kwanza kuusoma na hapo utaona kama kuna makosa yoyote. Kadhalika kwenye matumizi yako ya mitandao ya kijamii, kuwa makini na mwangalifu sana.
 
Back
Top Bottom