Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20200621-WA0032.jpg
 
Siwezi kuwateua Watu kisha Wamekaa wanabishana tu ndiyo maana nimesema RC,DC, DED Arusha wapumzike kwanza na hili liwe fundisho kwa viongozi niliowateua, mkajenge element za kuvumiliana kama unataka kubishana nenda kabishane nyumbani kwako na Mke wako" - JPM • • “Mkuu wa Mkoa Arusha ukasimamie migogoro, kuna migogoro mingine inatengenezwa makusudi, kaisimamie vizuri, mfano kulikuwa na mgogoro pale wa kanisa na shule kuna maamuzi hayakuwa ya kweli, nikawaambia wakitaka eneo wajenge ghorofa,Jiji haliwezi kuingia gharama kutafuta eneo”-JPM • • “Kulikuwa na mgogoro wa Msikiti Arusha, eneo lao ni mita za mraba 10,495 na open space mita 4165, kuna kiongozi mmoja akawa anawaambia ombeni na hili eneo DED alipokataa shida, ni kumchonganisha DED na Waislamu na hili lilianza tangu enzi za Mwinyi,Mkapa, Kikwete wakakataa na mimi msimamo wangu ni uleule nakataa”-JPM • “Tatizo hili (la migogoro Arusha) lililetwa na Mkuu wa Mkoa Arusha(Gambo) anazungumza hivi huku, anazungumza hivi kule lengo ni kuonekana yeye ni mzuri sana, tusitoe ahadi ambazo haziwezekani lazima tusimamie Sheria, RC, DC na DED msiende kuingia kwenye matatizo”-JPM
 
Nitamshangaa sana IGP kama ataondoka hapa aende akagombee Bunda akiomba ubunge akitegemea nitamteua kuwa waziri kwasababu ningetaka awe waziri si ningemteua tu kwenye nafasi za wabunge lakini nilimteua awe IGP wa Tanzania nzima kwanza hana uhakika kama atashinda kwenye kura za maoni na inawezekana akashinda bado nikamfuta, itategemea na siku hiyo nimeamkaje,” – Ameyasema Haya Mh Rais Maguindanao, JPM
 
Nitamshangaa sana IGP kama ataondoka hapa aende akagombee Bunda akiomba ubunge akitegemea nitamteua kuwa waziri kwasababu ningetaka awe waziri si ningemteua tu kwenye nafasi za wabunge lakini nilimteua awe IGP wa Tanzania nzima kwanza hana uhakika kama atashinda kwenye kura za maoni na inawezekana akashinda bado nikamfuta, itategemea na siku hiyo nimeamkaje,” – Ameyasema Haya Mh Rais Maguindanao, JPM
It must be overwhelming kuwa na madaraka makubwa kiasi hiki. Ukiamka vibaya tu unafuta watu na kuwaharibia maisha yao
 
Anza na mazungumzo binafsi kabla ya mazungumzo ya biashara. Unapokutana na mteja kabla hujaingia kwenye mazungumzo ya biashara, anza kwanza na mazungumzo binafsi, hili linajenga mahusiano mazuri lakini pia linakupa kujua kinachowasukuma wateja na kukusaidia kwenye mauzo.
 
Njia bora ya kupata mkutano na mtu yeyote ni kutumia mtandao wa kijamii wa LinkedIn, kuangalia kitu ambacho mnacho kwa pamoja na mtu unayetaka kukutana naye, labda mnatokea eneo moja, au mmesoma shule au chuo kimoja, kisha mtumie ujumbe ukijitambulisha na kueleza kile kinachowaunganisha na omba mkutano. Wengi watakuwa tayari kukupa nafasi.
 
Kujiamini kunaleta ubobezi. Jiamini sana kwenye kile unachofanya na watu watakuamini na kukuona ni mbobezi kwenye kile unachofanya. Unapojiamini unauza zaidi kwa sababu watu wengi zaidi wanakuamini. Jiamini lakini usiwe na kiburi.
 
Michezo ni moja ya mazungumzo ambayo kila mtu anaweza kuendana nayo. Unapokutana na mtu, jua anapendelea mchezo gani na anashabikia timu gani, hapo mnaweza kuwa na mazungumzo mazuri yanayojenga mahusiano mazuri kabla hamjaingia kwenye mazungumzo ya kibiashara.
 
Vaa kama mtu ambaye tayari ameshafanikiwa. Watu wanakuhukumu kwa mavazi na mwonekano wako. Hivyo mara zote kuwa na mwonekano mzuri, vaa kama mtu aliyefanikiwa. Mara zote vaa kama ambavyo wale unaotaka kufikia mafanikio yao wanavyovaa. Kama umeajiriwa, vaa kama anavyovaa bosi wako au mkurugenzi wa kampuni hiyo.
 
Tumia vizuri vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Hizi ni fursa za kuitangaza biashara yako na kuwafikia wengi bure kabisa au kwa gharama ndogo. Pata nafasi za kushiriki na kuhojiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na hilo litawafanya wengi zaidi wajue kuhusu wewe na biashara yako.
 
FIKIRI TOFAUTI.

Nenda kinyume na kundi la wengi na utafanikiwa zaidi. Kitu kinapofanywa na wengi, wewe fanya kinyume nao, na utafanikiwa sana. mara nyingi kinachofanywa na wengi siyo kitu sahihi. Mfano kwenye uwekezaji wakati kila mtu anauza, wewe nunua, na wakati kila mtu ananunua, wewe uza.
 
Endesha biashara yako kama kampuni ndogo mara zote. Kampuni ikishakuwa kubwa urasimu unakuwa mwingi na ugunduzi na ubunifu unapungua. Unapoendesha biashara yako, hata kama ni kubwa kiasi gani, iendeshe kama biashara ndogo, maamuzi muhimu yafanywe na watu wachache na yafanywe haraka.
 
Back
Top Bottom