Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Fikiri kwa akili yako kabla hujafanya maamuzi. Kuna watu wengi ambao wanashauri vitu vingi kuhusu biashara na uwekezaji. Lakini kamwe usifanye kitu kwa sababu ya ushauri wa wengine, kaa chini na fikiri kwa akili yako na ufanye maamuzi ambayo ni sahihi kwako.
 
Tengeneza jukwaa. Mfumo wa biashara umebadilishwa kwa kasi sana na ujio wa mtandao wa intaneti. Njia bora ya kuwa na biashara yenye mafanikio ni kuifanya biashara yako kuwa jukwaa ambali watu wanakutana. Na hata unapowekeza, wekeza kwenye kampuni ambazo ni jukwaa. Kampuni kubwa ya Amazon ni jukwaa ambalo wauzaji na wanunuzi wanakutana. Mitandao ya kijamii ni majukwaa ambayo yanakusanya watu na kuuza matangazo. Tengeneza jukwaa na utaweza kufanikiwa sana.
 
Usiheshimu mazoea, heshimu ugunduzi na ubunifu. Biashara nyingi zinakufa kwa sababu ya kufuata mazoea hata pale mambo yanapobadilika. Usiwe mtu wa kufuata mazoea, badala yake fuata ubunifu na ugunduzi mpya, kila kitu kinabadilika, biashara yako pia inapaswa kubadilika.
 
KUWA WEWE.

Kuwa mwaminifu na ongea kutoka ndani ya moyo wako. Unapokuwa unaongea na mtu yeyote, ongea ukweli na ongea kutoka ndani ya moyo wako. Kwa njia hii utaaminika na kuwashawishi wengi zaidi. Unapoongea kutoka ndani ya moyo wako watu wanajua wewe ni mtu halisi na siyo mwigizaji.
 
Usitoe nafasi kwa watu au mawazo hasi kwenye akili yako. Usiruhusu kabisa hali ya kushindwa au kukata tamaa iingie ndani yako. Usipokuwa makini, wewe mwenyewe utakuwa ndiyo kikwazo kwa mafanikio yako, kwa kujikosoa sana mwenyewe. Ondokana na mawazo hasi na ya kukatisha tamaa na usiyape nafasi kabisa kwenye akili yako.
 
Jipe muda wa kuwa na wewe peke yako. Huwa tunatoa muda wetu kwa kila mtu kasoro sisi wenyewe. Hakikisha unatenga muda wa kuwa wewe peke yako, kuyatafakari maisha yako, kuangalia unakotoka, uliko na unakokwenda na hata muda wa kupumzika pia. Wewe ndiye mtu muhimu kwako, jipe muda wa kuwa peke yako na kujisikiliza.
 
Hujachelewa kuanza chochote. Kwa zama tunazoishi sasa, unaweza kuanza kitu chochote kwenye umri wowote na bado ukafanikiwa. Kama ulichelewa kuanza, usijikatishe tama kwamba huwezi kuanza sasa. Kwenye umri wowote ule, unaweza kuanza chochote unachotaka kuanza na ukafanikiwa. Iwe ni biashara au ujuzi fulani, unachohitaji ni mapenzi na kuwa tayari kujifunza.
 
Kuvurugwa kunaleta ugunduzi mpya. Kuvurugwa kwenye kazi na hata biashara ni hali ya kawaida. Kuna wakati unafika na kuona kila unachofanya hakieleweki au kuchoshwa na namna mambo yanavyofanywa. Hapo ndipo pazuri kwa sababu unakuwa kwenye hatua nzuri ya kuja na ugunduzi mpya. Unapojikuta kwenye hali ya kuvurugwa, fikiria njia mpya na bora ya kufanya kile unachofanya.
 
Sawasawa
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…