By Zamaradi Mketema afunguka ujumbe unaotajwa kujaa busara kuhusu tifu la Shilole na Uchebe
''Mwanamke ni kiumbe wa thamani sana, lakini mara nyingine thamani hizi tunazipoteza wenyewe kwa kukubaliana na ushenzi na unyanyasaji mbalimbali na kujidanganya ndio uvumilivu kwa hofu tu ya kuiogopa jamii ambayo haitakuwepo pale athari mbaya zitapotokea, tumeshuhudia idadi ya vifo vingi siku za hivi karibuni vinavyotokana na matukio ya namna hii na baadae kutamkwa kwa urahisi tu kuwa “NI BAHATI MBAYA”, bahati mbaya inayoshindwa kumrudisha aliepotea na hata kuziba pengo kwa wahusika
Binafsi tumeongea mengi sana leo lakini kubwa fahamu maamuzi uliyoyaamua HAKUNA WA KUKULAUMU maana mzigo ni mzito kwa alieubeba, umekiri kuwa sio chini ya mara kumi ishirini kupokea kichapo cha Mbwa mwizi, nikijifanya vumilia ndio maisha ntakuwa mnafki, kama wewe umeona inatosha kazi yetu kama ndugu zako ni kukupa moyo na nguvu ya kusimamia ulichokiamua MWENYEWE na sio otherwise, Haya ni maisha yako na wewe ndio unajua zaidi hivyo kama umeona imetosha ni wewe, hawa washauri wote hawatakuwepo hata pembeni ya wanao pale utakapotoweka Duniani (TUMEYAONA NA TUNAISHI NAYO)
Ndoa ni masikilizano na maelewano, ndoa ni Upendo lakini NDOA NI HESHIMA, anaekuheshimu hawezi kuwaza kufanya hili tena mbele za watu mara nyingine, huenda una makosa yako kibinaadamu lakini bado haimpi haki ya kunyanyua mkono, teke, ngumi juu yako, Uvumilivu tuliofundishwa sio huu, na hata SHIDA NA RAHA zinazosemwa sio hizi, ni zile shida na raha zilizo ndani ya mapenzi na upendo, mlale njaa huku mkitabasamu, mfukuzwe kwenye nyumba huku mmekumbatiana, mpeane moyo wakati mnadhalilika kutafuta lakini sio nyinyi ndio mdhalilishane, hii iko kinyume na haki za Binaadamu hadi sheria za MUNGU,
Mwanzo nilikuwa na hofu na kuongea kwako, lakini nadhani UKWELI HUMUWEKA MTU HURU, na nimeshuhudia uhuru wako machoni leo, nawaombea wote kwa pamoja, MUNGU amnusuru yeye na mkono wa kupiga maana utamfikisha pabaya asipoangalia, lakini na wewe akuepushe na athari mbaya za vipigo
Jua tu UJASIRI WAKO UTAOKOA WENGI, kuna watakaopata nguvu kupitia wewe, na kuna wanaume watakaojirekebisha kupitia hili
Nawaza Hapo we ndio mtafutaji,vipi kwa wale wanaosubiria baba arudi ndio wale, tunapoona ya namna hii tujitahidi kuwa sauti kwa wasio nazo''