Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ndugu yangu. Mchakato wake ni mgumu sana. Inabidi uanze kujiimarisha huko jimboni kwa kusaidia jamii mapema ili ujulikane. Shida hata ukijaribu kufanya hivyo akina Joka Makengeza wanaanza kukuchunguza. Yupo jamaa yangu MD Bingwa wa magonjwa ya watoto alianza kujenga vituo vya afya kwa ajili ya watoto pale Wilayani. Alitaka kituo cha pale Wilayani kiwe chenye hadhi sana na yeye awe anakwenda kila mwaka mara mbili na jopo la madaktari wenzake na kutoa huduma bure. Alipigwa vita mpaka akabwaga manyanga. Akaamua kulitoa jengo bure napo akakataliwa. Aliishia kuwapa ndugu zake nao hawakujua wafanye nini. Lipo mpaka leo limekuwa pagale.

Siyo rahisi kamanda. Na bila pesa za kutosha hufiki po pote....
Njoo Dar nikupe jimbo la uchaguzi.
Hapa utafanikiwa maana hakuna mambo ya kuchunguzana sana
 
Njoo Dar nikupe jimbo la uchaguzi.
Hapa utafanikiwa maana hakuna mambo ya kuchunguzana sana
Siasa siziwezi kamanda. Usitishwe na makelele yangu humu. Kiuhalisia siyo mwongeaji sana na wala siyo social kivile. Ni mimi na mishe zangu tu. Sasa hii ya kuanza kujikomba kwa watu na unafiki itakuwa mtihani sana. Siasa zina wenyewe. Hata wewe nahisi unaziweza sana tu, kama haumo ndanimwe tayari. Na ubaya/uzuri hamsemagi. Si ajabu tunapishana mabarabarani huko mnatumwagia matope mkiwa ndani ya ma V8 yenu ya serikali. Shwaini zenu [emoji51][emoji51][emoji51]
 
#February2017

GWAJIBOY: Mimi siwezi kugombea ubunge kwa sababu nitakuwa nimejishusha chini. Ubunge kwangu ni demotion. Mimi ni mkubwa kuliko mbunge, mimi ni mkubwa kuliko Waziri, Mimi ni mkubwa kuliko Rais. Sema Amen.

WAUMINI: Ameeeeen.!

#July2020
GWAJIBOY: Itoshe tu kusema sasa nagombea ubunge jimbo la Kawe. Kuna watu wanasema eti ubunge ni kujishusha chini. Ngoja niwapasue sasa.

WAUMINI: Pasuaaaaa.!

GWAJIBOY: Ubunge sio kujishusha chini ni kupanua huduma, sema kupanua.

WAUMINI: Kupanua.

GWAJIBOY: Kupitia kanisa nilikua nafikia watu wa Dar es Salaam peke yake, lakini kupitia ubunge nitafikia taifa zima sasa. Napanua huduma. Sema kupanua.

WAUMINI: Kupanua.!
Aseeee.
Panuaaa panuu, panua tena.
Mchungaji huyo!
 
Back
Top Bottom