Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1596044850601.jpg
 
Kuna reply alicheka pasipo stahili... Imeumiza sana.
Unauguza mgonjwa, muuguzaji hauna matumaini ya mgonjwa wako kupona, mgonjwa nae anajua hawezi kupona, kwa upendo mkubwa muuguzaji unamfariji mgonjwa wako... "pole sana mama/baba yangu, Mungu yupo nasi utapona tu",mgonjwa anacheka huku anakuangalia kwa macho ya kuaga, anakushukuru kwa kumuuguza...[emoji24][emoji24][emoji24]

Pumzikeni mahali pema peponi wote mlio tangulia mbele ya haki [emoji120][emoji120]
AIsee sina comment Anko!
 
Alikosa msahauri.
Wakati mwingine JF si mahala pazuri pa kupata ushauri thabiti.
Nimesoma thread yake moja na sikuona kama alipata alichokihitaji ni mzaha tu na hata yeye alifanya reply za mzaha kwa swala ambalo ni serious sana kwake.
Mtu aliyeamua kujiua hata umshauri vipi ni kazi bure. Tena ukimaliza kumshauri atakushukuru vizuri sana na kukuhakikishia kuwa ameachana na hilo wazo kumbe ndiyo mnaagana jumla.

Ukisoma nyuzi zake huyu zinaonyesha alikuwa na matatizo mengi kuanzia alcoholism, madeni, kudharauliwa na wenzake, ishu za mapenzi, Bodi ya Mikopo na kukata tamaa. Ushauri wa hapa JF usingefua dafu labda professionals kabisa na hata wa kitabibu. Na guilty feelings kwa walioachwa ni jambo la kawaida mtu akijiua. Mnaachwa na maswali mengi. Pengine ningemshauri hivi, au ningefanya hiki labda asingejiua lakini ukweli ni kwamba mtu mzima akishakata shauri kabisa kabisa ni ngumu sana kumkinza...

Ila naona jamaa wameanza kuhoji kuwa aliyeleta tangazo la kifo yawezekana akawa ndiye marehemu mwenyewe kwa sababu kila kitu chao kinafanana. Naomba iwe hivyo na uzi wa kifo uwe ni njia nyingine ya kuomba msaada. Na ikiwa kweli basi utawala hapo UDOM wachukue hatua madhubuti kumsaidia mapema kabla hajajiua kweli [emoji1545][emoji1545]

Je, mleta taarifa siyo Umomi mwenyewe?
 
Back
Top Bottom