Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BreakingNews: Watu 10 wamefariki dunia na wengine 100 wakiokolewa, baada ya Boti iliyokuwa ikitokea maeneo ya Sibosa kupigwa na dhoruba kisha kugonga mwamba na kupasuka kisha kuzama ndani ya Ziwa Tanganyika. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP James Manyama amethibitisha.
 
Donald Trump ametoa wito kuwa uchaguzi wa rais utakaofanyika Novemba uahirishwe akidai kuongezeka kwa upigaji kura kwa njia ya posta kunaweza kusababisha udanganyifu na matokeo yasiyo sahihi. Kuna ushahidi mdogo wa madai ya Bwana Trump lakini kwa kipindi kirefu amekuwa akipinga upigaji kura kwa njia ya posta ambao anadai unaweza kusababisha udanganyifu. Majimbo ya Marekani yanataka upigaji kura kwa njia ya posta kufanywa kuwa rahisi zaidi kwasababu ya wasiwasi wa matatizo ya kiafya kutokana na janga la corona. Katika ujumbe wake kwa njia ya Tweeter, Bwana Trump amesema kupiga kura kwa njia ya posta kutafanya uchaguzi wa Novemba kuwa usio sahihi na wenye udanganyifu mkubwa katika historia ya nchi hiyo na aibu kubwa kwa Marekani. Alisema hivyo bila kutoa ushahidi wowote kwamba kupiga kuta kwa njia ya posta kama inavyofahamika Marekani, kutahatarisha uchaguzi kuingiliwa na nchi za kigeni. "Wanazungumza kuhusu uchaguzi kuingiliwa na nchi za kigeni lakini wanajua kwamba upigaji kura kwa njia ya posta ni njia rahisi ya nchi za kigeni kuuingilia," amesema. Bwana Trump alisema njia hiyo tayari unadhihirisha kwamba hilo litakuwa matatizo tu katika maeneo ambayo imejaribiwa
 
Mwisho wa wiki hii Rapper Tekashi *6ix9ine atakuwa mtu huru kabisa kwa mara ya kwanza tangu alivyokamatwa karibia miaka miwili iliyopita kwa makosa ya uhalifu na kutumia silaha kinyume cha sheria akihusishwa na makosa ya kundi lake la kihuni la kipindi icho 'Nine Trey Gang' Tekashi 6ix9ine anategemea kuachiwa huru jumapili hii (Aug. 2) baada ya kutumikia kifungo chake cha nje (nyumbani) kwa miezi minne baada ya kuachiwa mapema kutoka gerezani kwa hofu ya kupata maambukizi ya corona. Mwezi uliopita alijitoa tena kwenye mitandao ya kijamii, TMZ wameripoti kuwa kwasasa anaimarisha ulinzi wake kuhakikisha usalama wake anaporudi uraiani na ili kuhakikisha usalama wake wakati akitumia masaa 300 aliyopangiwa na mahakama ya kazi za kijamii.
 
Back
Top Bottom