Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuta ulizojiwekea katika maisha:
Pili unatakiwa uondoe "kuta" ulizojiwekea wewe mwenyewe katika kupiga hatua zaidi za kimaisha. Soma vizuri, nimesema katika kupiga HATUA zaidi za KIMAISHA. Sio katika KUTAFUTA maisha. Kuta hizo ni kama vile uwoga wa kushindwa, Uwega wa Maumivu, Uvivu na Kujitegemeza kwa wengine.
 
Ni kweli ni mara ngapi umeweza kufanikiwa katika jambo ambalo hapo awali ulidhani usingeliweza ? Na je, ni wapi uliona mafanikio yamekuja bila kuwepo na mapungufu katika njia ya kufikia mafanikio hayo? Utajiuliza, sasa ikiwa makosa nitajaribu na kushindwa nitakuwa nimepoteza vingi sana, itakuwaje ? Swali hilo bado linadhibitisha kuwa unao uwoga. Amini kuwa baada ya kushindwa, kutatokea njia mbadala au utakuwa umejifunza zaidi ili usikosee tena.
 
400019600733_278380.jpg
 
Uvivu ni adui yako mkubwa, hata hivyo pengine umemkaribisha na amekuwa kama sehemu ya wewe. Unachotakiwa kutambua ni kuwa ili mambo yafanyike ni lazima YAFANYIKE, hakuna cha ziada, hivyo basi FANYA, usiwe mtu wakusema NITAFANYA. Ni vema kuanza kidogo kidogo kuliko kusubiri majuto, ya kujiambia "ningejua".
 
Jambo lingine ambalo unafanya pengine kila siku ni kujishusha bila kukusudia. Mara ngapi ungeweza kujisomea ili kupata ufahamu fulani hata hivyo ukajiambia 'aah ntamuuliza fulani', mara ngapi ungeweza kujiwekea akiba ili kutimiza kusudio lako la kununua kitu fulani hata hivyo ukajisemea "aah ntamuomba fulani". Yaani hata haupati shida ya kujiuliza kama kweli hayo unayodhani wengine wafanye kwa ajili yako wewe mwenyewe unaweza kufanya. Hali hii ni pacha wa kufikia wa UVIVU.
 
Pengine hata wewe umewahi kuutumia tena bila hata kutafakari maana yake hasa ni nini, kwani utaishije maisha yako, wakati upo bize unayatafuta hayo maisha ? Si wewe peke yako, wengi wamekumbwa na hali hii kwakuwa tumefundishwa na kuaminishwa katika jamii zetu kutokuishi maisha yetu. Angalia matangazo ya biashara yanavyokuhamasisha kununua bidhaa fulani fulani.
 
Hivyo unajikuta na wewe umekuwa wa kuiga, umejifunza kujikataa, umejifunza kutokuangalia nini hasa unataka, bali nini haswa marafiki, ndugu na jamaa wanataka au wanategemea wewe uwe vipi. Halafu ukiitafakari hali unaona ni kama vurugu kwani hakuna anayeishi maisha yake.
 
Back
Top Bottom