Tunafahamu kwamba Uingereza inaongozwa kifalme na kimalkia, na malkia wa sasa wa Uingereza ni Elizabeth II aliyeingia madarakani mwaka 1952, kabla yake alikwepo mfalme George VI ambaye alivyofariki tuu ndipo akaingia Elizabeth. Kabla ya George VI kulikuwepo na mfalme Edward VIII aliyetawala kwa muda wa miezi 12 tuu kati ya January 1936 na December 1936, huyu aliacha ufalme mwenyewe na kuandika historia ya kuwa mtawala wa kwanza wa Uingereza kuachia ufalme kwa hiari yake mwenyewe. Kwanini Aliacha? Kisa ni mapenzi. Ilikuwaje? Edward alikuwa mtoto wa mwisho katika familia, baba yake George V ndiye alikuwa mfalme wa Uingereza, na alikuwa anampenda sana mwanaye huyu hadi kufikia kusema wazi kuwa akifariki yeye basi mwanae huyu wa mwisho ndiye arithi ufalme. Ni kweli baada ya baba yake kufariki January 20, 1936 Edward VIII akaingia madarakani kama mfalme mpya, lakini wakati anaingia alikuwa ameanza kupendana na mwanamke wa kimarekani Wallis Simpson ambaye walikuwa wanajuana tangu miaka mitano nyuma. Edward alitaka kumuoa Wallis, lakini shida ikaja kwa familia na viongozi wengine wa nchi wakisema kuwa Uingereza haiwezi kuwa na malkia kutoka Amerika, kwahivyo Edward hawezi kumuoa mrembo huyo wa kimarekani. Ilifika kipindi Edward alishutumiwa kuwa anataka kumuoa mwanamke wa kimarekani na kumfanya malkia ili kuiangamiza Uingereza, walihofia anaweza kuwa mpelelezi aliyetumwa kuichunguza Uingereza, hii ilipelekea kujihuzuru kwa viongozi wengi wa serikali. Edward aliona isiwe tabu, baada ya kukaa miezi 12 madarakani December 11, 1936 akaamua kutangaza rasmi kuwa anaachia kiti cha ufalme ili awe huru kumuoa mwanamke anaempenda huku akisema kuwa hawezi kuwa mfalme bila yeye, ni kweli aliacha, na Juni 7, 1937 wakaoana. Kaka yake George VI ndiye alichukua kiti cha ufalme ambapo naye baada ya kuariki mwaka 1952 akamuachia ndugu yake Elizabeth II ambaye ndiye malkia hadi sasa. Edward alifariki mwaka 1972 na Wallis alifariki mwaka 1986.