Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kesho yake March 1, 2000 John aliwaaga kazini rafiki zake kuwa kama kesho yake hatafika kazini basi wajue kuwa mkewe atakuwa amemuuwa, alipoombwa asirudi nyumbani kwa mkewe huyo alisema kuwa anarudi tuu kwasababu anahofia atawauwa watoto.
 
John alikuwa anawapenda sana watoto, licha ya kuwa hawakuwa watoto wake, wote wanne walikuwa ni watoto wa mwanamke aliowapata katika ndoa zake zilizopita, Kathe aliwahi kuachana na mwanaume saa chache tuu baada ya kufunga nae ndoa.
 
Usiku huo ndio alioutumia kumuuwa mumewe huyo, alimchuna ngozi na kumpika kabla ya baadae kuwafuata watoto wake na kuwapa msosi huo wa nyama ya baba yao. Polisi walifika na kumkamata siku moja baadaye. Hadi sasa yupo jela, ana miaka 64.
 
Bhagar alikuwa kijana mzalendo, askari aliyekuwa mstari wa mbele kuongoza mapambano ya kuudai uhuru wa nchi yake ya India kutoka kwa Uingereza, uongozi wake katika mapambano hayo ukapelekea anyongwe na wakoloni hao March 23, 1931 akiwa na miaka 23 tuu.
 
Wakati wazazi wanamlazimisha aoe alikataa katakata akisema kuwa hawezi kuoa katika ardhi ya nchi yake iliyo chini ya wakoloni, kama ataoa basi kifo chake ndo kitakua mahali yake, alikimbia nyumbani kisa kulazimishwa kuoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…