Che alikuwa mwanaharakati na mwanamapinduzi halisi. Fikiria baada ya mapinduzi ya Cuba kufanikiwa pamoja na kupewa uwaziri lakini baadaye aliukataa akidai kuwa kuna sehemu nyingi watu masikini na wasio na nguvu walikuwa wakiendelea kuonewa. Huyoo sehemu mbalimbali duniani kwenye migogoro huku akipigana na kutoa misaada ya kitaalamu ya kimikakati na hata kitiba. Mpaka Kongo huku na hata kuuawa katika mistu ya Bolivia huko. Kuna mini documentary hapa ilikuwa inaonyeshwa na Smithsonian channel na majasusi wa CIA waliohusika kumsaka walikuwa wanaelezea harakati zao. Lakini mpaka wananyanyua bastola kumtandika risasi ya kichwani tena mchana kweupe kauli yake ya mwisho ikawa ni kwamba mnachoweza ni kuua tu mwili wangu lakini fikra zangu zitabaki. Wanamapinduzi wa aina hii ni nadra sana kuwapata!
Na shida mojawapo kubwa ya Nyerere ilikuwa ni kukosa wafuasi wa kweli wa itikadi na mawazo yake. Alikuwa amezungukwa na kundi la wanafiki tu waliokuwa wanamwogopa sana kumbe lengo lao kuu ilikuwa ni matumbo yao. Baada ya kifo chake ndipo ukweli ulikuja kubainika. Hata mwanafunzi wake mwenyewe aliyemwamini sana mpaka akafikia kuzunguka nchi nzima akimpigia kampeni za urais aligeuka na kuwa bepari tena mwenye tamaa kweli kweli ya mali. Akina Komredi Kingunge - wajamaa wa kupigiwa mfano wale kumbe walikuwa na chembe chembe za ubepari...
Sifa mojawapo kuu ya viongozi waliofanikiwa kuwa na fikra zilizodumu mpaka kubadilisha maisha ya jamii zao vizazi na vizazi ni kuwa na wafuasi wa kweli wa itikadi na falsafa zao. Vinginevyo inageuka na kuwa one man show tu na siku kiongozi huyo akiondoka madarakani watu wanaendelea na mambo yao. Hiki ndicho kilichoziangusha fikra za Nyerere. Na ndicho kitaiangusha hii Magufulification inayoendelea kwa sababu sidhani kama ana wafuasi wa kweli.