Hakika, kazi yangu nayofanya sasa ni matunda ya wema niliofanya mwaka 2014 kwa mtu ambae sikuwahi kujua kama anaweza kulipa kwa namna hii.Siyo wazazi tu. Na watu baki pia.
Mimi nililipiwa karo kidato cha kwanza mpaka cha nne na mtu baki tu. Alichotaka nifanye ni kuwa namtumia matokeo yangu ya kila muhula na makubaliano yetu yalikuwa kwamba lazima niwe kwenye top ten. Na kweli sikumwangusha. Ameanza kuzeeka sasa na mwaka jana tulifanya sherehe nyumbani kwake tukacheka na kufurahi. Nami nimejivika jukumu sasa la kusomesha watoto wake watatu kwa vile yeye kiuchumi hajiwezi tena - na masharti ni yale yale. Watoto wasiwe nje ya top 10. Maisha haya. Ni mtihani mzito sana tena kuzidi ule wa Cambridge lakini matendo mema tunayowafanyia wenzetu - hata kama hawatakuwa na uwezo wa kutulipa - ndiyo kipimo halisi kabisa cha ubinadamu na utu wetu. Mungu na Akatusaidie [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Mwaka ule alipitia changamoto nyingi na hakuwa na kazi, hivyo nilichofanya mimi ni kuwa namtoa pesa kidogo na kumfanyoa application vile hakuwa na laptop (tulisoma wote chuo). Badae akapata lazi ya kawaida tu na mawasiliano yakabaki ya mara chache sana.
Ikawa imepita miaka kimya kimya, mwaka huu mwezi wa tano nikaona call yake, hata moyo ukalipuka sana. Akaniambia nimtumie email yangu personal, nikatuma thereafter nikaona offer letter ya kuitwa kazini.
Kuja kujua bhana yule dada kumbe ndio big boss aiseeee.