Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unique-places-to-visit-in-Africa-Uganda-Chimp-900x563.jpg
 
Hakika, maisha yetu ni mafupi sana. Muhimu tuwe watu wa kusaidia wenye uhitaji hata kwa msaada wa mawazo tu.
Hapa kituoni kwangu,kuna mtoto mwenye changamoto ya mwili (mlemavu) huwa anapenda kuja sana vile kuna ofisi nyingi maeneo haya.
Kiukweli ni mtoto ambae huwa ananiumiza sana nikimuona, sina uwezo mkubwa kifedha ila huwa nampa sana refreshments kama soda, biscuits au maji. Nikimpa yule mtoto huwa anafurahi sana, na akifurahi basi na mm huwa napata amani sana moyoni.
Huwezi amani wkend huwa natumia muda mwingi sana kumuwaza yeye kuliko hata watoto wangu, lakini jioni hii nimepata habari njema kuwa yule mtoto anahudumiwa sana na Plan international pamoja ma Help Age International.
Mara nyingi kama mzazi naumia sana nafikiria mtoto yule anatembea peke yake na hali yake ile, je usalama wake uko wapi?
So mara nyingi namsaidia, hata nikimkuta barabarani siwezi kuendelea na safari hadi nimtoe japo naumia sana.
Mazingira yangu ya kazi ni magumu mno kwa mtu alie na huruma kama mimi. Huwa nikirudi kwangu, nikikumbuka nalia sana kwa uchungu.
Wajua nini bageshi. Furaha, amani na ridhiko la kweli linapatikana kwa kusaidia wengine, hasa wale ambao hawawezi kuurudisha wema huo. Na wengi wanaamini kuwa maana hasa ya maisha yetu imefichwa humo.

Kuna documentary moja hapa nilikuwa naangalia ya tajiri mmoja huko India. Yeye alikuwa na tabia ya kutoa pesa tu kwenye mashirika mbalimbali yanayojihusisha na kusaidia watoto wenye ulemavu. Shirika mojawapo likatumia pesa zake kujengea darasa la vitu practical kwa watoto hawa ili wapate ujuzi fulani utakaowasaidia maishani. Basi siku ya ufunguzi wa hilo darasa viongozi wa shirika hilo wakasema lazima awepo kwa sababu watoto walikuwa wanataka kumuona na kumshukuru. Anasema kuwa alikuwa hataki kwenda na alikwenda tu kwa shingo upande na baada ya kushawishiwa sana.

Anasema alipotambulishwa kuwa ndiye yeye aliyetoa pesa za kujenga darasa lile na ndiyo huwa anatoa pesa za chakula chao watoto wale wenye kila aina ya ulemavu walikuja kumkumbatia na kumshukuru sana huku wakilia. Walimpa pia na barua waliyokuwa wameiandika. Anasema siku ile alilia sana kama mtoto mdogo mpaka wasaidizi wake wakamshangaa kwa sababu ni mtu mkali sana na asiyecheka wala kuonyesha hisia. Anasema tukio lile lilibadilisha maisha yake na lilimwonyesha hasa maana ya maisha ni nini. Na barua ile aliyopewa siku ile ameitunza vizuri kwenye frame na kuiweka ofisini kwake. Anasema kuwa kila anapojisikia kuchoka na hata kukaribia kukata tamaa barua ile humpa nguvu na kumrejeshea matumaini.

Hata kwenye msiba wa Marehemu Mengi, mbali na mbwembwe zote, wengi waliguswa sana na watoto waliokuwa wakimlilia kwa sababu ya misaada aliyokuwa akiwapa. Kumbe alikuwa anasomesha na kusaidia watoto wengi wenye ulemavu na wenye shida. Leo hii matajiri wakubwa akina Bill Gates na wenzake wame-pledge kutoa zaidi ya nusu ya fedha zao ili ziende huko zikasaidie wengine...

Asante kwa msaada wako kwa mtoto huyo. Bila shaka umeacha alama ya kudumu katika maisha yake. Na hakuna wema unaopotea bure dadangu. Mibaraka hiyo itakurudia tu kama siyo wewe mwenyewe basi wanao. Endelea kupanda hizo mbegu njema. Matunda yake ni ya kudumu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Hii picha nimejikuta namkumbuka Anko binti mpole...
Popote ulipo Anko Esta hawayuu[emoji137][emoji137]
Huko kaliko si ajabu kanapaliliziwa nyasi. Au labda tu kanafanya zile tafiti zisizo na kichwa wala miguu. Shwaini za kenyewe [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
 
Back
Top Bottom