Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1607782090101.jpg
 
Aseee.
Hongera kamanda.
Pole pia kamanda.

Ila usifadhaike sana maana "kila nafsi itaonja kifo".
Kamanda, pamoja na furaha tuliyonayo hapa tunapokutana na kutaniana, kumbuka kuna siku isiyojulikana tutaachanishwa na KIFO.
Mungu muumba mbingu na ardhi na vile vilivyomo ametukutanisha hapa tutaniane, tucheke na tufurahi, lakini malaika wa mauti yupo nyuma yetu.

Basi ukawe na siku njema kwenye siku yako hii muhimu.
Mungu akupe umri mrefu
Ukae mahali pa utulivu muombee mambo mazuri yamfikie marehemu mama huko aliko
Asante sana ndugu yangu. Maneno ya hekima mno. Ndiyo. Binadamu huwa tunajisahaulisha mpaka tunafikia hatua ya kutendeana ubaya na hata kuuana. Lakini ukiyaangalia maisha kwa upana wake, unaweza ukakosa hata maana yake halisi. Mungu Atupe neema zake na Atupe maarifa na uwezo wa kuwa karibu naye na kutenda yale yanayompendeza. Muda wetu ni mfupi sana [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Mungu Wangu, sijui nilikua wapi sijaona hii, Happy Birthday Super Dad,brother, friend, family and a blessing to many, Mungu akutunze, may you live to blow 10000 candles, i love you Dadii
Asante sana mpendwa japo hii ID yako mpya imenipiga chenga aisee. I receive all your blessings and good wishes. Mungu Atulinde [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Shemeji yangu kipenzi. Nilikuwa sijaona hii. What a surprise jamani [emoji1545][emoji1545][emoji1545]

Ndiyo. Ni siku ya ajabu hii. Ni siku ya kuumba na kuumbua. Mama aliamua kunileta hapa duniani katika siku hii. Halafu hapo hapo naye akaamua kuiacha dunia hii katika siku hii hii. Ni siku yenye mixed feelings sana kwa kweli!

Nakumbuka miaka mitatu nyuma siku kama ya leo nilipoweza kuagana na mama kwenye simu. Sauti yake ilikuwa imara mpaka dakika za mwisho. Alikuwa na amani na hakuwa katika mateso. Ooh maagano yale!

Nakumbuka jinsi ulivyosimama imara kunitia moyo. Nakumbuka nilivyosafiri kwa haraka haraka na kukuta kijiji kizima na ukoo wote wakinisubiri kwa ajili ya mazishi. Kumbe mama kabla hajakata roho alimnong'oneza dada kuwa ni lazima wanisubiri kitinda mimba wake nije nimuage. Japo sina lo lote wala cho chote lakini mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa kidunia na kiroho walifika kumuaga mama. Ushahidi wa kuishi vyema na watu!

Nimeandika sana. Umegusa sana hisia zangu shemeji. Hebu undugu, wema na ubinadamu wetu tulioujenga hapa na ukadumu daima. Tunapokoseana tusameheana. Nina deni kwako sana na sijui nitalilipaje. Tuombe uzima shemeji yangu kipenzi [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Pole sana, nimejikuta napata msisimko fulani hivi wa huzuni.
 
Back
Top Bottom