Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hongera wakulima wote..
FB_IMG_1607655863273.jpg
 
Happy bday SHIMBA YA BUYENZE najua leo ni siku ambayo ina mixed feelings kwako.
Nina mengi ya kukuombea kwa Mungu.
U mtu wa tofauti sana,nimepata bahati ya kuwa kati ya wale wanaofurahia uwepo wako.
Naomba nichukue nafasi hii kukutakia kila lililo la kheri katika maisha yako.
Mungu akuinue zaidi ya hapo ulipo.
Akuongezee hekma,busara na furaha katika maisha yako,uishi miaka mingi kadiri ya mapenzi yake.
Happy bday shem darling[emoji322][emoji323][emoji323][emoji8][emoji8][emoji8]
Uzidi kubarikiwa siku zote

Shemeji yangu kipenzi. Nilikuwa sijaona hii. What a surprise jamani [emoji1545][emoji1545][emoji1545]

Ndiyo. Ni siku ya ajabu hii. Ni siku ya kuumba na kuumbua. Mama aliamua kunileta hapa duniani katika siku hii. Halafu hapo hapo naye akaamua kuiacha dunia hii katika siku hii hii. Ni siku yenye mixed feelings sana kwa kweli!

Nakumbuka miaka mitatu nyuma siku kama ya leo nilipoweza kuagana na mama kwenye simu. Sauti yake ilikuwa imara mpaka dakika za mwisho. Alikuwa na amani na hakuwa katika mateso. Ooh maagano yale!

Nakumbuka jinsi ulivyosimama imara kunitia moyo. Nakumbuka nilivyosafiri kwa haraka haraka na kukuta kijiji kizima na ukoo wote wakinisubiri kwa ajili ya mazishi. Kumbe mama kabla hajakata roho alimnong'oneza dada kuwa ni lazima wanisubiri kitinda mimba wake nije nimuage. Japo sina lo lote wala cho chote lakini mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa kidunia na kiroho walifika kumuaga mama. Ushahidi wa kuishi vyema na watu!

Nimeandika sana. Umegusa sana hisia zangu shemeji. Hebu undugu, wema na ubinadamu wetu tulioujenga hapa na ukadumu daima. Tunapokoseana tusameheana. Nina deni kwako sana na sijui nitalilipaje. Tuombe uzima shemeji yangu kipenzi [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Happy birthday The don, Nakuombea Neema na baraka tele maishani, Siku zote usiache kutushauri vijana wako popote tunapohitaji msaada Wako... hata mimi nafurahia uwepo wako na nashukuru kukufahamu!.[emoji7]
Asante sana TH. Sina wasiwasi na wewe. You are going places malaika wa watu wewe [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Back
Top Bottom