Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Happy bday SHIMBA YA BUYENZE najua leo ni siku ambayo ina mixed feelings kwako.
Nina mengi ya kukuombea kwa Mungu.
U mtu wa tofauti sana,nimepata bahati ya kuwa kati ya wale wanaofurahia uwepo wako.
Naomba nichukue nafasi hii kukutakia kila lililo la kheri katika maisha yako.
Mungu akuinue zaidi ya hapo ulipo.
Akuongezee hekma,busara na furaha katika maisha yako,uishi miaka mingi kadiri ya mapenzi yake.
Happy bday shem darling[emoji322][emoji323][emoji323][emoji8][emoji8][emoji8]
Uzidi kubarikiwa siku zote
Mungu Wangu, sijui nilikua wapi sijaona hii, Happy Birthday Super Dad,brother, friend, family and a blessing to many, Mungu akutunze, may you live to blow 10000 candles, i love you Dadii
 
Kuna Binadamu wanaletwa Duniani kwa ajili ya Binadamu wenzao, japo ni wachache na ni maskini kabisa lakini wamewekeza utajiri wa faraja kwenye Nafsi za watu wengi sana.
Mtenda mema hapa Duniani huinuliwa na wanadamu, kwa Mungu ni thawabu na pumziko lake ni Peponi.
Tumuombee maisha marefu yenye afya njema. Vile vile kale kabinti kake tukaombee katimize ndoto zake kaje katutibu uzeeni tezi nanihii...

Mungu akubariki Shimba [emoji120][emoji120]
Shemeji. Maneno mazito haya ila nayapokea kwa mikono miwili. Tumekuwa kama ndugu humu kabisa. ASANTE sana...

Jana nilikuwa kwa dentist. Nilikuwa na cavities mbili na ilibidi kuziziba. Basi wamenikorokochoa na hayo masindano yao basi hata raha ya kula hakuna japo kabinti kamejitahidi kupika.

Mungu Atulinde shemeji. Siku moja miye nitakuja kula ugali uliopikwa na Kabula wangu huko Masaki [emoji1545][emoji1545]
 
Shemeji yangu kipenzi. Nilikuwa sijaona hii. What a surprise jamani [emoji1545][emoji1545][emoji1545]

Ndiyo. Ni siku ya ajabu hii. Ni siku ya kuumba na kuumbua. Mama aliamua kunileta hapa duniani katika siku hii. Halafu hapo hapo naye akaamua kuiacha dunia hii katika siku hii hii. Ni siku yenye mixed feelings sana kwa kweli!

Nakumbuka miaka mitatu nyuma siku kama ya leo nilipoweza kuagana na mama kwenye simu. Sauti yake ilikuwa imara mpaka dakika za mwisho. Alikuwa na amani na hakuwa katika mateso. Ooh maagano yale!

Nakumbuka jinsi ulivyosimama imara kunitia moyo. Nakumbuka nilivyosafiri kwa haraka haraka na kukuta kijiji kizima na ukoo wote wakinisubiri kwa ajili ya mazishi. Kumbe mama kabla hajakata roho alimnong'oneza dada kuwa ni lazima wanisubiri kitinda mimba wake nije nimuage. Japo sina lo lote wala cho chote lakini mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa kidunia na kiroho walifika kumuaga mama. Ushahidi wa kuishi vyema na watu!

Nimeandika sana. Umegusa sana hisia zangu shemeji. Hebu undugu, wema na ubinadamu wetu tulioujenga hapa na ukadumu daima. Tunapokoseana tusameheana. Nina deni kwako sana na sijui nitalilipaje. Tuombe uzima shemeji yangu kipenzi [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Aseee.
Hongera kamanda.
Pole pia kamanda.

Ila usifadhaike sana maana "kila nafsi itaonja kifo".
Kamanda, pamoja na furaha tuliyonayo hapa tunapokutana na kutaniana, kumbuka kuna siku isiyojulikana tutaachanishwa na KIFO.
Mungu muumba mbingu na ardhi na vile vilivyomo ametukutanisha hapa tutaniane, tucheke na tufurahi, lakini malaika wa mauti yupo nyuma yetu.

Basi ukawe na siku njema kwenye siku yako hii muhimu.
Mungu akupe umri mrefu
Ukae mahali pa utulivu muombee mambo mazuri yamfikie marehemu mama huko aliko
 
Hakuna mkulima hapo...ungesema bilionea wa madini labda [emoji16][emoji16][emoji16]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkulima wa jembe la mkono
FB_IMG_1607782074680.jpg
 
Happy birthday kwake kaka yangu, Shimba mwenyewe.
Mwenyezi Mungu azidi kukupa miaka mingi zaidi uzeeke hadi uwe wa kubeba. Ila uzeeke ukiwa na hela[emoji1][emoji1][emoji1].
Uzidi kujaaliwa maisha marefu na yenye Baraka, kupitia kwako tuzidi kujifunza mengi.
Ujaaliwe hekima kama za Mfalme Suleiman na uzidi kupewa kibali cha kuinuliwa na kukubalika kama cha Samweli.
Asante sana dadangu mwema. Hebu sala yako hii na ikapate kibali machoni pa Mungu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Shemeji. Maneno mazito haya ila nayapokea kwa mikono miwili. Tumekuwa kama ndugu humu kabisa. ASANTE sana...

Jana nilikuwa kwa dentist. Nilikuwa na cavities mbili na ilibidi kuziziba. Basi wamenikorokochoa na hayo masindano yao basi hata raha ya kula hakuna japo kabinti kamejitahidi kupika.

Mungu Atulinde shemeji. Siku moja miye nitakuja kula ugali uliopikwa na Kabula wangu huko Masaki [emoji1545][emoji1545]
Happy Birthday To You [emoji512][emoji512] [emoji173][emoji173]
 
Back
Top Bottom