Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa sehemu kubwa, wamasai wanaishi kwa kutegemea maziwa na nyama ya mifugo yao. Hivi ndivyo wanavyopata virutubisho vya protini na karoli.Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wamasai wameongeza aina nyingine za vyakula katika mlo wao: chakula cha mahindi, viazi, mchele na kabichi.
 
Ingawaje Kulingana na jadi, jambo hili halikubaliwi. Hii ni kwa sababu wamasai wanaona kutumia ardhi kwa ajili ya kilimo cha mazao ni kama uhalifu n ani kinyume na uoto wa asili kwa vile inafanya ardhi isifae kwa malisho ya mifugo.
 
Na hapo kuna damu! Wamaasai hunywa damu katika matukio mbalimbali: wanapokuwa wagonjwa, punde tu wanapotahiriwa au punde tu wanapojifungua. Baada ya Ilamerak (neno la kimasai linalohusu wazee ) pia hunywa damu kuzuia uchovu baada ya kunywa kilevi
 
Sio tu kwamba damu ina protini nyingi, ni nzuri pia kwenye mfumo wa kinga. Hata hivyo idadi ya mifugo inapopungua, hamu ya damu inakuwa ndogo. Hii ni hakika moja wapo ya ukweli wa kabila ya Kimaasai.
 
Wamasai wameitwa kutokana na lugha yao wenyewe.

Jina Masai kifasihi humaanisha “mtu anayeongea lugha ya Maa”. Lugha yenyewe ni sehemu ya tawi la watu wa Naili (Neolithic) mashariki ya familia ya lugha ya Nilo- Sahara.
 
Pia ni kawaida kwa watu wa kimasai kuwa na matobo makubwa masikioni. Hii ni kawaida ya makabila mengi kama unavyoweza kuona katika picha za makabila mengine. Walakini, wamasai ufanya tofauti kidogo. Wakati makabila mengi uziba na mbao walipotoboa, wamasai ujaza matobo yao makubwa na shanga pamoja na hereni moja ya kuambatanisha kimtindo.
 
Aisee....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…