Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vitu vingine vya kuzingatia kuhusu ndoa za kimasai ni kwamba mwanamke huwa ni mdogo zaidi ya mumewe. Hii umaanisha kabila la kimasai lina wajane wengi. Hawategemei kuolewa tena, jukumu la mwanamke katika ndoa umasaini ni kuzaa na kuwa na watoto.
 
Hii ufahamika kama Enkipukonoto Eaji ambayo inatafsirika kama ” kutoka katika kipindi cha kutengwa”. Kabla ya sherehe, mama na mtoto utengwa na kuruhusu nywele kuota kuwa ndefu. Unyolewa baada ya sherehe. Hii ni ishara ya mwanzo mpya kwa mtoto.
 
Wamasai wana kalenda yao wenyewe.Tarehe za msimu wa kimasai.Kalenda ya kimasai inaweza changanya kidogo kutokana na kwamba hamna sheria za kimataifa zinazohusu majina ya miezi 12 wala maelewano juu ya mwezi upi ufata upi,” japo kila mtu anajua kuna miezi 12 na siku thelathini za kila mwezi. Siku 15 za mwanga na siku 15 za giza na siku ya 8 ujulikana kama ” siku ya kubadilika”
 
Kwa sababu hio, mchanganyiko mwingine ujitokeza mwishoni mwa kila mwezi ambapo siku mbili za mwisho wa mwezi zina mabishano kutokana na kwamba mwezi ” umekwisha chukuliwa” au kama ” bado” haujachukuliwa. Kuna misimu mikuu 3: mvua za muda mrefu, msimu wa manyunyu, na mvua za muda mfupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…