Katika hatua za mwisho,Leicester imeamua kuweka mipango ya kumchukua kwa mkopo mlinzi na kiungo wa kati wa Arsenal na England Ainsley Maitland-Niles. Wakati huohuo Southampton, West Brom na Newcastle wanamuwania mchezaji huyo, 23. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 28, ambaye amehusishwa na kurejea Tottenham, huenda akasalia Inter Milan hata baada ya siku ya mwisho ya uhamisho Jumatatu na kuwa na jukumu muhimu sana katika timu hiyo, amesema mtendaji mkuu wa klabu ya Italia Giuseppe Marotta. (Sky Sports)
Aliyekuwa kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumchukua mlinzi wa Uhispania na Real Madrid Sergio Ramos, 34, na kumpeleka Paris St-Germain. (Independent)
Beki wa kati wa RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 22, huenda akajiunga na Ligi ya Primia mwaka huu huku maajenti wake wakisema kuwa hivi karibuni atachagua kati vilabu viwili vya Uingereza vilivyo "juu" na Bayern Munich (Mail)
Kiungo wa kati wa Tottenham Tanguy Ndombele, 24, amesema mchezaji mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, amejaribu kumshawishi ajiunge naye Paris St-Germain. (Goal)
West Brom inataka kusajili wachezaji wawili siku ya mwisho ya uhamisho na inamkodolea macho mlinzi Okay Yokuslu, 26, wa Uturuki kutoka Celta Vigo na beki wa kulia wa Uingereza Japhet Tanganga, 21, kutoka Tottenham. (Express and Star)
Newcastle United inafuatilia kwa karibu usajili wa kiungo wa kati wa Uingereza anayechezea Leicester City Hamza Choudhury, 23, katika makubaliano ya mkopo hadi mwisho wa msimu. (Chronicle)
Burnley inataka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Josh King, 29, siku ya mwisho ya usajili ingawa mshahara ndio huenda ukawa kikazwo. (Lancashire Telegraph)
Manchester City inajadiliana na Fluminense kuwasajili viungo wa kati wa Brazil, 17, Kayky na Metinho, lakini klabu hiyo ya Amerika Kusini inataka zaidi ya pauni milioni 15. (Mail)